Na Mwandishi Wetu
WANAFUNZI waliomaliza kidato Cha nne mwaka 1995 katika shule ya sekondari Kidia iliyoko mkoani Kilimanjaro wamechangia zaidi ya sh mil 20 kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa La Kiinjili La Kiluther Tanzània (KKKT) usharika Wa Kidia.
Wanafunzi hao wametoa mchango huo kama shukrani na sadaka kwa Mungu kwa kuwawezesha kutumia usharika huo kwa kipindi chote walichosoma shuleni hapo lakini pia wakitumia usharika huo kwa shughuli mbalimbali ikiwemo za kielimu na kiroho pia.
Mchango huo wa ujenzi pamoja na Zawadi mbalimbali ambao ni Sadaka ulikabidhiwa kanisani hapo Agosti 10,2025 katika ibada iliyoongozwa na Mkuu wa pili Wa Jimbo La Kilimanjaro Kati ambaye pia ni Mchungaji Kiongozi Usharika Wa Majengo, ,Mchungaji Israel Moshi,akishirikiana na Mchungaji Kiongozi Usharika Wa Kidia Mchungaji Sayuni Shao pamoja na Mchungaji Kiongozi Usharika Wa Kirua Mchungaji James Sambo.
Akizungumza Mwenyekiti wa Umoja Wa Wanawake Wakatoliki Tanzania ( WAWATA) na RAIS Wa Wanawake Wakatoliki Afrika , ambaye ni miongoni mwa wanafunzi waliomaliza kwa kipindi hicho, Evaline Malisa Ntenga alisema wanafunzi hao sio kitu bali neema ya Mungu waliyoiita wakati wakimaliza kidato Cha nne mwaka 1995 ndio iliyosababisha kurudi mahali hapo na Kutoa sadaka hiyo.
"Wako wanafunzi wengi waliotamani kufika bali sisi ni wawakilishi wao," Alisema na kuongeza kuwa ni alama ya shukrani kwa Mungu maana imepita miaka 30 tangu kumaliza kidato Cha nne.
Aidha alisema anashukuru wazazi waliowalea wanafunzi hao na kwamba huo ni wito kwa wazazi nchini Kuwekeza Kwenye malezi.
Aliyekuwa Kaka Mkuu wa shule kwa kipindi hicho,Hendry Kandore alikabidhi majina ya wanafunzi 119 walioanza safari ya masomo shuleni hapo kipindi hicho.
Kwa upande wake Mchungaji Moshi aliwapongeza wanafunzi hao kwa kukumbuka wakati wanasoma na kwamba Uwezo na nguvu za Mungu ziwapiganie katika Maisha Yao kwa Utume waliofanya.
"Tunawapongeza sana, historia mlioacha haitosahaulika kamwe," alisema Mchungaji Moshi huku akiwataka kuendelea kuikumbuka shule ya Sekondari Kidia ambayo bado inaendelea kutoa huduma.
Hata hivyo Mchungaji wa Usharika huo ,Shao aliipongeza kundi hilo kwa jitijada kubwa walizoonesha Kuichangia ujenzi wa Kanisa hilo.
" Ni kweli washarika wanaendelea kuongeza juhudi na ujenzi umefikia ngazi ya kuweka madirisha eneo balo hata hawakujua ingekuwaje lakini Mungu amewatumia kutimiza jambo hilo," alisema Mchungaji Shao aliyejawa na furaha wakati wote.
Kundi la wanafunzi hao lilitimiza safari ya miaka minne shuleni hapo mwaka 1995 likijumuisha wanafunzi 119 miongoni mwao wakitoka vijiji tofauti tofauti zaidi ya tisa ambao walitumia muda mrefu kutembea kwa ajili ya kuisaka elimu na kufanikiwa kuwa katika taaluma mbalimbali nchini.
0 Comments