Na Magrethy Katengu , Dar es salaam
SERIKALI kupitia Kituo Cha Uwekezaji Nchini (TIC) kimepokea wawekezaji wapatao 25 kutoka Nchini Qatar ambao wamekuja nchini kwa lengo la kuangalia fursa zilizopo za Uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo,Utalii,tiba, usafirishaji ambapo itasaidia kuchochea uchumi kukua zaidi na zaidi
Ameyasema hayo leo Jijini Dar es salam Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Anna Lyimo amesema ujio wa wawekezaji hao ni matokeo chanya ya ziara iliyofanywa hivi karibuni na Viongozi wa TIC ambao walienda nchini Qatar nakufanya mazungumzo na baadhi ya Wafanyabiashara kutoka shirikisho la Wafanyabiashara la Qatar KERALA BUSINESS FORUM.
" Ujio wa wageni hao ni jitihada zinazofanywa za kuhamasisha na kwenda Nchini kwao kufanya ziara na kufanya mazungumzo kuieleza Tanzania ilivyo na kuwavutia wawekezaji,hivyo kusaidia wawekezaji wapatao 25 kuja kuangalia fursa ya kuwekeza Katika sekta mbalimbali ikiwemo Mifugo,Vifaa tiba,Utalii,Madawa, sekta ya anga pamoja na masuala ya uchumi wa Bluu" amesema Anna.
Hata hivyo amesema kutokana na kuwepo kwa diplomasia nzuri ya Uwekezaji pamoja na kufungua milango kwa wawekezaji hao wawekezaji wengi wa kigeni wameanza kujitokeza huku akiwasihi wawekezaji wa ndani wajiunge na TIC waweze kupata taarifa mbalimbali za fursa ya Uwekezaji Wanaotoka nje ya Nchini.
Sanjari na hayo amesema kuwa wawekezaji hao wanatarajia Machi 29 kutembelea Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuangalia fursa ya Uwekezaji lakini kwa Sasa TIC inawapitisha katika taratibu mbalimbali za Uwekezaji pamoja na masuala ya vibali vya namna kuwekeza Nchini.
Kwa upande wake Raisi wa Shirikisho la wafanyabiashara Nchini Qatar Bw.Shanavas Bava amesema Tanzania ni Nchi iliyobarikiwa na Mwenyezi Mungu kuwa na hali ya hewa nzuri na ina utulivu na amani hivyo wamekuja kuangalia fursa zakuwekeza
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Lanchi ya Taifa( NARCO) Bw. Petter Msofe amesema mazao mengi ya Mifugo Kama vile nyama ya Mbuzi,Ng'ombe na Kondoo yamekuwa yakitumika sana Mjini Doha Nchini Qatar hivyo wawekezaji hao watasaidia kikuza sekta ya Mifugo nakuongeza pato la Taifa.
" Hivi karibuni tulihudhulia mkutano mkubwa wa Kilimo na Mazingira uliyofanyika mjini Doha Nchini Qatar,tulishirikiana na ofisi ya balozi wa Tanzania Nchini Qatar,Doha wanapenda sana kula nyama inayotoka kwetu hivyo wawekezaji wameanza kuja kuwekeza, na sisi tunaendelea kuunga Mkono serikali ya rais Samia Suluhu Hassan ambaye ameonyesha nia ya kufungua milango ya uwekezaji"amesema bwana Msofe.
0 Comments