WAZIRI AIAGIZA NIMR KUSAMBAZA DAWA ZAKE ZA ASILI KWENYE MADUKA YA DAWA MAKUBWA KILA MKOA


Na Asha Mwakyonde, DODOMA 

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, ameitaka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), kuonekana sokoni kunapopatikana huduma za dawa mbadala, miti shamba Pamoja na kwenye maduka makubwa ya dawa kila Mkoa.

Hayo amesema leo Juni 17,2025 jijini hapa katika maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2025 yenye Kaulimbiu isemayo "Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidijitali Kuongeza Upatikanaji wa Taarifa na Kuchagiza Uwajibikaji" amesema kuwa NIMR ni chombo cha Taifa na kwamba ni jambo jepesi kuwepo sokoni ambapo ikifanya hivyo dawa zitanunuliwa.


Kwa upande wake Mtafiti Mwandamizi kutoka NIMR Dk. Akili Kalinga amesema kuwa wanatafiti magonjwa mbalimbali ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza ambapo majibu ya utafiti huo wanaishauri Wizara ya Afya namna ya kufanya matibabu kutikanana na tafiti hizo.

"Tunatafiti za magonjwa mengi yakiwamo magonjwa ya Sukari, moyo  saratani ambayo ni magonjwa yasiyo ya kuambukiza pamoja na kufanya utafiti katika magonjwa ya kuambukiza kama malaria, kifua kikuu na magonjwa mapya yakiwamo ya mfumo wa hewa," ameeleza.

Akizungumzia dawa mbadala amesema ni dawa ambazo zinasaidia kutibu wananchi huku akisema kihistoria watu wa wazamani walizitumia dawa hizo.

Dk. Kalinga ameongeza kuwa taasisi hiyo imejikita katika kutafiti dawa hizo zikiwamo za  Nimrevit, Nimricaf ambayo ilikuwa ikitumika wakati wa kutibu, kukinga  Kirusi ambacho husababisha Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19),

"Dawa hizi tumeshauriwa na Waziri Simbachawene tuhakikishe zinasambaa katika maduka ya dawa makubwa na zifike mahala ambapo wananchi wanaweza kuzifikia kwa urahisi," amesema Dk. Kalinga.

Amefafanua kuwa dawa hizo zinatokana na tafiti tofauti na zile za waganga wa kienyeji ambao wanasema bila kufanya utafiti.

Post a Comment

0 Comments

TAWA YAPOKEA TUZO KUTOKA KWA TAASISI YA FOUNDATION FOR DISABILITIES HOPE (FDH)