CPB YASAINI MIKATABA NA KAMPUNI NNE ZA KUNUNUA MAZAO

Na Asha Mwakyonde

BODI ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania (CPB),imesaini mkataba na kampuni nne za wazawa za kununua mazao zikiwamo Ngine General Suppuls, Izina  Farm Limited na MT and David Company Co.

Haya yamesemwa katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara  ya Dar es Salaam maarufu Saba Saba yaliyofikia tamati Julia 13,2022 yaliyokuwa yakifanyika kwenye  viwanja vya  Mwalimu Julius Nyerere jijini hapa na Meneja wa Masoko wa Bodi hiyo Fred Mbilinyi amesema kuwa wamenufaika na maonyesho hayo kwa kuwa wamepingia makubalino na kusaini mikakata na kampuni nne za kununua mazao.

Meneja huyo amesema wamesaini mkataba huo wa kununua mazao na kwamba Bodi hiyo wananunua mazao mchanganyiko kutoka vyama vya ushirika kwa wananchi mbalimbali nchi nzima.

"Bodi ya Nafaka Mchanganyiko Tanzania tupo Kanda tano ambazo Dar es Salaam, Dodoma ambayo ndio makao makuu, Kanda ya Ziwa, Nyanda za juu Kusini Iringa na Mtwara. Tupo nchi nzima kila sehemu tunanunua mazao kutoka kwa wakulima wa Tanzania," amesema.

Amesema wao kama Bodi wameona wananchi wengi wamejitokeza kwenye mabanda yao kuangalia bidhaa walizonazo na kwa kuwa wananunua kutoka kwa wakulima Watanzania hatua hiyo imewasaidia kupata wateja wengi wa nchi mbalimbali kutembelea mabanda hayo na kutamani kufanya nao biashara.

" Siku ya mwisho ya kuhitimisha maonesho ya Saba Saba sisi kama Bodi ya Nafaka tumenufaika na maonyesho haya kama kaulimbiu inavyosema 'Tanzania Ni Sehemu Sahihi ya Biashara na Uwekezaji'," amesema.

Ameongeza kuwa Bodi hiyo ina viwanda ambavyo inavimiliki hivyo watu wengi wamejitokeza hasa kuangalia  vinavyochakata mashindi kuwa unga wa Dona na sembe na viwanda vya kuchakata ngano na vya alizeti.

"Tuna waambia Watanzania kama Rais Samia Suluhu Hassan anavyosema kazi Iendelee nasi tuna sema tupo chini ya Wizara ya Kilimo mwaka huu tunajambo letu,"ameeleza.

Awali akizungumza mara baada ya kusaini na Bodi hiyo mmoja wa kampuni hizo  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni  Ngine General Suppuls Lathifah Chande ambayo amesema kuwa wamefarijika na mkataba huo ambao unawaweka katika sehemu nzuri baina yao na CPB.

" Ni sehemu nzuri ya kuanzia ya kuwa na malengo makubwa  hii yote inatokana na maonesho haya. Kupitia jukwaa la wanunuzi na wauzaji wa mazao mbalimbali ndipo tulipoingia kwenye mkataba huu na kufanya maamuzi ya kuuziana bidhaa ya Soya," amesema.

Ameongeza kuwa wameingia mkataba wa tani tatu  kwa kuwa ni mwanzo wanatarajia kufikisha tani 10,000 za Soya  huku akisema kwamba kampuni hiyo ni moja ya kampuni ambazo zimesajiliwa kuuza mazao nchini China.

Post a Comment

0 Comments

DKT. BITEKO ASISITIZA UMUHIMU WA MIFUMO THABITI YA NISHATI JADIDIFU KUKIDHI MAHITAJI YA NISHATI