TAWA YAWAVUTA WANANCHI SABASABA KUFUNGA MWAKA KWA BURUDANI NA ELIMU YA UHIFADHI

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam 

WANANCHI wanaendelea kumiminika katika Viwanja vya Sabasaba, Kilwa Road jijini Dar es Salaam kushiriki Tamasha la Kufunga Mwaka Kijanja na Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania(TAWA),linaloendelea katika viwanja hivyo hadi Januari 05, 2026.

TAWA inawakaribisha wananchi wote kujitokeza kwa wingi ili kuburudika, kuelimika na kujifunza kuhusu uhifadhi wa wanyamapori pamoja na vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo chini ya usimamizi wa taasisi hiyo. 

Aidha, washiriki watapata fursa ya kununua na kumilikishwa nyara halali za Serikali zikiwemo ngozi za simba, chui, fisi na nyinginezo.

Vilevile, tamasha hilo linatoa fursa adimu ya kuonja nyama choma za wanyamapori, kupiga picha na taswira za wanyamapori wa aina mbalimbali, na kubaki na kumbukumbu isiyosahaulika.




Post a Comment

0 Comments

UTABIRI WA HALI YA HEWA SAA 24 ZIJAZO Disemba 28,2025