TAASISI ZA UTAFITI ZATAKIWA KUUNGANA


 NA ASHA MWAKYONDE, MBEYA

WAZIRI wa Kilimo Dk. Mashimba Ndaki amezitaka Taasisi za utafiti kuungana pamoja kufanya tafiti mbalimbali ambazo zitaleta manufaa kwa wafugaji na wakulima.

Taasisi hizo ni Taasisi ya Utafiti wa 
wa Kilimo Tanzania (TARI),na Taasisi ya Utafiti wa  Mifugo (TALIRI).

Dk Ndaki amesema hayo jana wakati akitembelea mabanda ya maonyesho ya Taifa ya wakulima Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakalinga vilivyopo jijini hapa.

Amesema taasisi hizo zikiungana pamoja zinauwezo wa kufanya vizuri katika masuala ya utafiti ambayo wanafanya kila siku.

"Taasisi hizi zikiungana pamoja zitafanya kazi vizuri kwenye masuala ya utafiti,"alisema Dk Ndaki.

Dk. Ndaki ameeleza kuwa  zaidi ya kuwa taasisi hizo zinaweza kushirikiana katika kufanya utafiti kwenye masuala ya malisho ya mifugo na kuweza kupata bora ambayo itaisaidia wafugaji kupanda malisho bora kwa ajili ya mifugo.

Kwa upande wa masuala ya mbegu hivyo hivyo aliwataka kushirikiana pamoja ili kuhakikisha wanapata mbegu bora ambazo zitaleta manufaa kwao na taifa kwa ujumla.

Naye Mkurugenzi wa wa TARI Dk.Geofrey Mkamilo amesema taasisi hiyo imejipanga kuhakikisha wanafanya tafiti bora ambazo zitatoa manufaa kwa wakulima na taifa kwa ujumla.

Dk Mkamilo amesema tayari wamezisambaza mengi za migomba katika mikoa mbalimbali ili waweze kutumika na wakulima.

Alifafanua zaidi ya kuwa mbegu hizo zitasaidia kumtoa mkulima kwenye hatua moja kwenda nyingine kutokana na kuzaliana kwa wingi pale inapopandws kulingana na maelekezo.

"Hii mbegu ya migomba ni nzuri sana wakulima wanapaswa kuitumia maelekezo ya maafisa ugani ili wapate mazao mengi.

Hata hivyo alisema wanafanya pia utafiti kwenye udongo ili kujua ni ufongo upi ambao unafaa kwa zao husika na eneo husika.

Kwa upande wake Dk Catherine Semkondo alisema wao kama TARI wako mstari wa mbele kuhakikisha utafiti unafanyika kwenye mbegu ili kuhakikisha wanalima sehemu sahihi.

Amesema mbali na utafiti wa mbegu wamekuwa wakiangalia masuala ya udongo ili kutoa nafasi kwa wakulima kulima eneo sahihi kwa mazao sahihi.

Post a Comment

0 Comments

BARABARA YA LAMI YA KM 7.7 YENYE THAMANI YA BILIONI 9.3 KUUNGANISHA MIKOA YA SINGIDA-SIMIYU-ARUSHA