Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) Dk.Michael Ng’umbi, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za taasisi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Oktoba 24,2022 jijini Dodoma.
NA ASHA MWAKYONDE, DODOOMA
TAASISI ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) imefanikiwa kuwafikia wasichana 3,333 sawa na asilimia 111 ya lengo ambao walishindwa kuendela na sekondari kutoka na mazingira magumu, kupata ujauzito na ndoa za utotoni.
Hayo yasemwa Oktoba 24, 2022 jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo
Dk.Michael Ng’umbi, amesema kuwa waliendesh mafunzo kwa nyakati tofauti kwa wasimamizi na watendaji, wawezeahaji na walimu wa madarasa ya mradi wa SEQUIP.
Amesema taasisi hiyo imehamasisha kurejea shuleni wasichana walioshindwa kuendelea na elimu ya sekondari kupitia vituo 131 vinavyohudumiwa na walimu 803.
"Katika mwaka 2021/2022 TEWW kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF), imetekeleza mpango wa elimu changamani kwa vijana walio nje ya shule (IPOSA) ukiwa na vituo 85 vyenye wanufaika 12000 na walimu 290 katika mikoa 9 ya Tanzania bara," ameeleza Dk.Ng'umbi.
Ameongeza kuwa mpango huo umelenga maeneo manne ambayo ni stadi za kisomo, stadi za ufundi, wa awali,stadi za maisha na stadi za ujasiliamali.
Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa TEWW imeendelea kutekeleza programu ya IPPE ambayo ni mpango wa elimu chanagamani baada ya elimu ya msingi ambao una wanafunzi 842 katika mikoa 11 huku akisema Taasisi hiyo itahamasisha kusajili na kufundisha wanafunzi 3000 wa mradi wa SEQUIP kwa mwaka 2023.
Dk. Ng'umbi amesema kuwa wanatarajia kupanua mpango wa IPOSA katika mikoa 6 mipya kwa kujenga karakana za kufundishia na pia kupanua mafunzo ya tehama kwa wanafunzi katika mpango huo IPOSA.
Pia amevitaja vipaumbele vya taasisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/ 2023 kuwa ni pamoja na kuimarisha usajili na usimamizi wa watoa huduma za elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi katika ngazi ya elimumsingi kwa kuboresha mfumo mzima wa usimamizi na ufuatiliaji, ikiwa ni pamoja na kuimarisha mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji wa takwimu.
Ameongeza kuwa ni pamoja na kuimarisha uendeshaji na utoajai mafunzo kwa walimu na wasimamizi wa elimu ya watu wazima nchini kwa kuboresha mifumo ya tehama na kuimarisha uandaaji mitaala, mihtasari na machapisho yanayohusu elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi na kuwa na machapisho bora na kwa wakati.
0 Comments