NA ASHA MWAKYONDE, DODOOM
BODI ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB), ina mpango wa kuanza kutumia teknolojia ya kuzalisha mafuta ya kupikia yatokanayo na pumba za mpunga kupitia kiwanda chake cha Mkuyuni mkuyuni jijini Mwanza.
Akizungumza na Waandishi wa habari Oktoba 24,2022 Jijini Dodoma Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko [CPB] DKT Anselm Moshi amesema sasa wapo katika upembuzi yakinifu katika kuongeza thamani mazao ya mpunga ili kuweza kuzalisha mafuta yatokanayo na pumba za mpunga.
Aidha,Dkt.Anselm amesema bodi hiyo ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ina mpango wa kuzalisha kuni kupitia pumba za Mpunga katika kupunguza uharibifu wa mazingira.
Dkt.Anselm amesema kwa mwaka 2021 taasisi hiyo imefanikiwa kununua mazao tani elfu sitini na nne .
Ikumbukwe kuwa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB), ni Taasisi ya serikali chini ya wizara ya Kilimo iliyopewa dhamana ya kufanya biashara ya nafaka na mazao mchanganyiko na imeanzishwa kwa sheria ya nafaka na mazao changanyiko Namba 19 ambapo pia hadi sasa mzunguko wa biashara katika taasisi hiyo umeongezeka kutoka bilioni 15 hadi bilioni 52
0 Comments