ZAIDI YA BILIONI 46 KUTUMIKA KUWALIPA WALIONDOLEWA KAZINI


 NA  ASHA MWAKYONDE,DODOMA


JUMLA  ya shilingi bilioni  46.8 9 zimetolewa na serikali  kwaajili ya kuwalipa Watumishi walioondoleewa kazini kwa vyeti feki zinatotokana makato ya mifuko ya hifadhi ya jamii ambapo NSSF ni asilimia 10, pamoja na PSSF asilimia 5.

Pia waajiri wametakiwa kuhakikisha  wanazingatia misingi ya utumishi wa Umma na Utawala Bora zoezi hilo kwa kuwa watumishi hao ni haki yao hawatakiwi kupata fedha hizo kwa bugudha yoyote.

Akizungumza jijini Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira, na wenye Ulemavu Prof.Joyce Ndalichako amesema Rais Samia ameridhia watumishi hao walioondolewa kazini kwa kughushi vyeti kurejeshewa michango yao waliyokatwa kwenye mishahara na kuwasilishwa kwenye mifuko ya jamii.

"Wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi  Mei mosi shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania ( TUCTA) kupitia risala yao waliwasilishwa ombi kwa mheshimiwa Rais aangalie namna ya kuwafuta jasho watumishi hao Rais alielekeza kufanyika kwa uchambuzi Ili kuona namna gani Serikali inaweza kuhitimisha suala hilo,

Prof. Ndalichako amesema kutokana na  uchambuzi uliofanyika Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia kuwa watumishi wote walioondolewa kazini kwa kughushi vyeti warejeshewe michango yao tuu waliyokatwa Kwenye mishahara na kuwasilishwa kwenye mifuko ya bifadhi ya jamii na kufuatia maelekezo hayo mifuko ya hifadhi ya jamii PSSF na NSSF itarejesha michango ya wafanyakazi iliyowasilishwa kwenye mifuko hiyo bila kuhusisha michango ya mwajiri.

Akizungumzia kuhusu watumishi waliofariki na wanapaswa kurejeshewa michango yao Profesa Ndalichako amesema wapo watu walioandikwa kwenye mirathi hao ndio watakaostahili kupatiwa fedha hizo.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama ameagiza waajiri wote wa mamlaka za Serikali za mitaa kuhakikisha wanazingatia maadili ya utumishi wa Umma na kuhakikisha kuwa kusiwe na mianya yoyote ya rushwa na kusema kuwa zoezi hilo ni haki ya watumishi hao walioondolewa kazini

"Waajiri wote mamlaka za Serikali za mitaa kufanya mambo yafuatayo,tunaagiza wawajibike Katika kutoa ushirikiano watakaohusika na zoez hili la watumishi,wahahakikishe wanaandaa madawati ya msaada kuna watu wanakuwa hawajui wakifika waende wapi.

Amesema kuwa wanaamini waajiri wataifanya kazi hiyo kwa weledi na uadilifu hatutarajii zoezi hilo kufanywa mradi kwa baadhi huku akiagiza TAKUKURU Kuanzia sasa wahahakikishe wanazingatia pasiwe na mianya ya rushwa.

Hata hivyo amesema waajiri ndio waliosimamia zoezi la kuwaondoa kazini hivyo wanauwezo kwakuwa nyaraka zote wanazo.

Ikumbukwe kuwa malipo hayo yanakuja baada ya shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) kupitia risala yao wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi  Mei mosi kumuomba Rais Samia aangalie namna ya kuwafuta jasho watumishi hao walioondolewa kazini kwa kughushi vyeti.


Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA