GAWIO LA SH. BILIONI 45.5 KWA SERIKALI LAPAMBWA NA BURUDANI

Na Eleuteri Mangi, WUSM Dar es salaam

SERIKALI imepokea gawio la Shilingi bilioni 45.5 kutoka benki ya NMB PLC ikiwa ni sehemu ya faida waliyopata katika mwaka 2022 ili kuboresha huduma za jamii nchini ikiwemo elimu na afya nchini kwa maendeleo endelevu.

Akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya kiasi hicho wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 25 ya mafanikio ya benki hiyo iliyofanyika Juni 17, 2023 jijini Dar es Salaam, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali imepokea gawio kubwa ambalo limetolewa na taasisi ya fedha nchini.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Bi Ruth Zaipuna amesema gawio las benki ya NMB kwa Serikali limeendelea kuongezeka kwa kiasi kikubwa na endelevu kutoka Shilingi Bilioni 4.5 mwaka 2009 hadi kufikia Shilingi Bilioni 45.5 mwaka 2022 sawa na ongezeko la asilimia 911 katika kipindi hicho cha mrejesho.

Katika kusherehesha hafla hiyo, burudani kutoka vikundi mbalimbali zilipata wasaa wa kuburudisha hadhira iliyofurika katika ukumbi wa Mlimani City akiwemo Msanii wa Music wa dance Christian Bella pamoja na vikundi vya ngoma. 

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, Mawaziri, Makatibu Wakuu akiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu pamoja na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania Nyakaho Mahemba.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU