DMI YAFANYA UDAHILI MAONESHO YA TCU MNAZI MMOJA


Na Asha Mwakyonde, Dar es salaam

CHUO Cha Bahari Dar es Salaam (DMI),kinafanya udahili wa moja kwa moja katika Maonesho ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), lengo likiwa ni kuwapunguzia wanafunzi gharama za mitandao kwa wanaohitaji kujiunga na chuo hicho.

Akizungumza jijini Dar es salaam Julai 18,2023 na Waandishi wa Habari Mkuu wa chuo hicho Dk.Tumaini Gurumo katika banda la DMI kwenye Maonyesho ya 18 ya TCU, yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja yenye kaulimbiu isemayo 'Kukuza Ujuzi Nchini kupitia Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia kwa Uchumi Imara na Shindani', amesema kuwa wanafanya udahili wa kozi mbalimbali zinazopatika chuoni hapo.

Dk.Gurumo ameemwataka wananchi kutembelea banda hilo ili kujua fursa za masomo zinazotolewa na chuo hicho na kuweza kufanya maamuzi ya kujiunga.

"Tupo hapa katika Maonesho haya lengo ni kutaka wananchi wajue fursa zinazopatikana katika chuo hiki ikiwa ni pamoja na kutoa elimu juu ya matumizi uokozi wa melini inapotokea dharura," ameeleza Dk. Gurumo.

Chuo hicho dira yake ni kutoa mafunzo ya hali ya juu yanayo endeshwa na mahitaji, utafiti na huduma za ushauri katika taaluma za baharini na taaluma zinazo husiana katika ukanda wa kusini mwa jangwa la Sahara na kwingineko.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI