UDOM KUANZISHA KOZI YA AKILI BANDIA


Na Asha Mwakyonde,Dar es salaam

CHUO Kikuu Cha Dodoma (UDOM), kimesema hivi karibuni kinatarajia kutoa kozi fupi ambayo inayohusu masuala ya  Akili Bandia (Artificial Intelligence), kutokana na kukua kwa teknolojia duniani lengo likiwa ni kuwaandaa Watanzania kwa kuwa teknolojia hiyo  imewakuta na haikwepeki.

Pia Chuo hicho kimesema kuwa  kina kozi mbalimbali zikiwamo zinazo watayarisha vijana ili waweze kujiajiri wenyewe badala ya kusubiri ajira kutoka serikalini na katika mashirika ya Umma na binafisi.

Akizungumza jijini Dar es salaam Julai 18,2023 na Waandishi wa Habari Makamu Mkuu wa UDOM, Profesa.Kuziluka Lughano wakati alipotembelea  banda la chuo hicho katika Maonesho  ya 18 Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja yenye kaulimbiu isemayo 'Kukuza Ujuzi Nchini kupitia Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia kwa Uchumi Imara na Shindani', amesema kuwa Akili Bandia ambayo inatikisa Dunia kimaendeleo badala ya kuteseka nayo wameamia  kuwaanda Watanzania kuitumia kwasababu imewatukuta.

Prof. Lughano ameeleza  Chuo hicho kinawataalamu ambao kwa sasa wanatoa maelezo kuhusu teknolojia hiyo ambayo inawachanganya Watanzania wengi.

Akizungumzia kozi zinazotolewa UDOM Prof. Lughano amesema wanatambua fursa za ajira sio nyingi na kwamba wanafuanzi wao wanaomaliza chuoni hapo wanauwezo wa kujiajiri wenyewe na kuajiri wengi kupitia kozi wanazozifundisha.

Makamu huyo wa Chuo hicho amesema ushiriki wao katika maonesho hayo unatoa fursa kwa wao kuzitangaza kozi wanazozitoa ambazo zinawatoa vijana katika dhana ya kusubiri kuajiriwa pamoja na shughuli mbalimbali wanazozifanya zikiwamo za utafiti ,machapisho,na maendeleo ya teknolojia.

"UDOM imekuwa ikifanya vizuri katika maeneo mbalimbali hususani katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA),na Sheria ambapo tumekuwa washindi katika Mashindano Barani Afrika," amesema Prof. Lughano.

Aidha amewakaribisha  wanafuanzi wanaotaka kujiunga na Chuo hicho kwa kuwa kuna Wataalamu waliobobea katika masuala mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU