GLOBAL EDUCATION LINK :TUPO TAYARI KUWASAIDIA WANAFUNZI WALIOKUWA WAKISOMA NCHINI SUDAN

Na Asha Mwakyonde, Dar es salaam

BAADHI ya  wanafunzi Watanzania waliokuwa wakisoma nchini Sudan  ambao walirudi Tanzania kutokana na mapigano nchini humo wametakiwa kutembelea banda la Taasisi ya Uwakala wa Vyuo Vikuu Nje ya Nchi (Global Education Link), ili kuweza kusaidiwa kwenda kusoma nchi nyingine kwa gharama ile ile.

Kutokana na mapigano hayo nchini Sudan Taasisi ya Uwakala wa Vyuo Vikuu Nje ya Nchi (Global Link) imeanzisha dawati maalumu kusaidia Watanzania hao ambao walirudi lengo likiwa ni kwamba Wasiendelee kupoteza, kwa muda kwani  hatujui machafuko yatakwisha lini.

Akizungumza jijini Dar es salaam Julai 18,23 na Waandishi wa Habari  katika banda la Taasisi hiyo kwenye Maonyesho ya 18 Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja yenye kaulimbiu isemayo 'Kukuza Ujuzi Nchini kupitia Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia kwa Uchumi Imara na Shindani', Mkurungenzi Mtendaji wa  Global Education Link, Abdulmalik Mollel, ameeleza kuwa wapo wanafunzi ambao wamerudi nchini na hawajui hatma ya masomo yao huko Sudan.

Mkurungenzi Mtendaji huyo amesema Global Link ipo tayari kuwasaidia wanafunzi hao ambao wanatamani kuendelea na masomo  nchi nyingine kwa gharama ile ile ikiwa wamejiridhisha kweli walikuwa wanasoma katika nchi hiyo.

Mollel amevitaka vyuo vikuu kuchangamkia fursa ya ushirikiano na vyuo vikuu vya nje 16 ambavyo vimeshiriki maonesho hayo kutoka katika nchi nane.

Mkurugenzi huyu ameeleza kuwa mwaka huu katika mabanda ya kampuni hiyo kuna baadhi ya Vyuo Vyuo vikuu vikiwamo kutoka Uturuki, India, Uingereza, British Council vimeshiriki maonesho hayo lengo likiwa ni kuwapatia fursa Watanzania kujua nini wanataka kuanzia ngazi ya diploma hadi shahada za Uzamivu ( PhD).

"Katika maonesho haya yalioanza Julai 17 na yanatarajiwa kumalizika Julai 22 mwaka huu, yanayoratibiwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU),chini ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia sisi kama Global Education Link kikubwa ni kupongeza jitihada za serikali hasa serikali ya wamu ya sita kwa kuwa tayari kuifungua Tanzania katika sekta ya elimu kupitia mikataba mbalimbali inayoendelea kusainiwa na Taifa la hili," amesema Mollel.

Ameongeza kuwa Global Education Link jukumu lao kubwa ni kuunga mkono  jitihada za serikali katika kuisaidia kuendelea kuifungua Tanzania kwenye masuala ya elimu ya juu kwa kushirikiana na Vyuo Vikuu vya kimataifa.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI