MU YAANZASHA PROGRAMU MPYA ZA KIMKAKATI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO


Na Asha Mwakyonde, Dar es salaam

CHUO Kikuu Mzumbe (MU),kimeanzasha programu tatu  mpya  ambazo zinawaandaa Wataalamu wa kusimamia miradi Maendeleo ya serikali ya kimkakati katika sekta za afya, mazingira na viwanda.

Akizungumza Jijini Dar es salaam Julai 18,2023 katika banda la chuo hicho Mratibu wa Udahili kutoka Chuo Kikuu Mzumbe Dk.Michael Mangula kwenye maonesho ya 18 Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja yenye kaulimbiu isemayo 'Kukuza Ujuzi Nchini kupitia Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia kwa Uchumi iImara na Shindani'.amezitaja programu hizo kuwa ni Shahada ya Utawala wa Umma katika Maendeleo ya Vijana na Uongozi (Bachelor of public Administration in youth Development and leadership), ambayo umeanzishwa mahususi na ni maelekezo ya serikali ya kuwaanda Wataalamu watakaosimamia Maendeleo ya vijana.

Dk. Mangula  amesema nyingine ni Shahada ya Kwanza ya Mfumo wa Afya katika ufuatiliaji wa Tathmini (Bachelor of Health System in monitoring Evaluation),ambayo ina waandaa Wataalamu wanaosimamia miradi kwenye sekta ya afya na nyingine ni Shahada ya Usimamizi wa Mazingira (Bachelor environmental Management),nayo inawaanda Wataalamu kwa ajili ya kusimamia shughuli za mazingira.


Ameongeza kuwa miradi mingi imekuwa sio endelevu hivyo kupitia programu hizo Wataalamu watapatikana  wa kusimamia miradi hiyo huku akisema chuo hicho kinakidhi mahitaji ya kizazi cha sasa bila kuathiri kinachokuja.

"Tupo hapa  kwenye maonesho ya TCU kwa lengo la kuwaelimisha wazazi na wanafunzi ambao wamemaliza kidato cha nne, cha sita na diploma tumefungua dirisha la Udahili kuanzia ngazi ya cheti, diploma, shahada za awali, (Bachelor degree) shahada za Umahiri (Masters), na shahada za Uzamivu ( PhD),nawakaribish kutembelea banda letu hapa Mnazi Mmoja ili kupata Udahili wa moja kwa moja ameeleza Dk.Mangula.

Dk. Mangula amesema kuwa kwa wanaofika kwenye banda hilo kwanza wanawaelimisha juu ya programu zinazopatikana katika chuo hicho pamoja na kuwaambia sifa zinahitajika ili mwanafunzi aweze kujiunga.

Ameeleza kuwa Chuo Kikuu Mzumbe kinatoa mafunzo ya muda mrefu katika maeneo mbalimbali ya ubobezi kwa upande wa sheria, utawala na menejimenti, biashara, ujasiriamali, uhasibu na fedha, uchumi na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA),Takwimu tumizi, Ualimu ,Usimamizi wa shughuli za uzalishaji viwandani, kuandaa wahandisi katika Usimamizi wa uzalishaji kwenye viwanda.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI