NIT YAONGEZA KOZI MPYA UHANDISI WA MITAMBO


Na Asha Mwakyonde Dar es salaam

KUTOKANA na ukuaji  Maendeleo ya Sayansi Teknolojia,Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), kimeanzisha kozi mpya ya Shahada ya Uzamili 'Masters' katika Uhandisi wa Mitambo lengo likiwa ni kuongeza wataalam wabobezi katika fani hiyo.

Akizungumza Dar es Salaam Julai 18,2023
Kaimu Ofisa Uhusiano wa chuo hicho,Juma Mandai katika banda la NIT kwenye  Maonyesho ya 18 Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja yenye kaulimbiu isemayo 'Kukuza Ujuzi Nchini kupitia Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia kwa Uchumi iImara na Shindani', amesema wanahitaji kuongeza wabobezi katika fani ya uhandisi wa mitambo.

Ameeleza  maboresho yanayofanywa na serikali katika sekta ya uchukuzi yanahitaji watalaam mbalimbali na kwamba NIT imeona fursa ya kuongeza kozi za ‘masters’ ili kupata wataalam wabobezi zaidi.


Aidha  amewataka Watanzania kuchangamkia kozi za kuandaa wataalamu wa kusimamia reli ya kisasa (SGR),wahandisi wa matengenezo ndege,wajenzi wa meli, usimamizi wa bandari,wahudumu wa ndege ambazo ni 
za kimkakati zinazozingatia mahitaji ya soko la ajira.

Ameongeza kuwa miradi mingi  ya kimkakati katika sekta ya uchukuzi inayoendelea kutekelezwa na serikali ya awamu ya sita inawahitaji  Watanzania waliobobea  kwenye masuala hayo.

"Tunawakaribisha katika banda letu tutawapa maelezo ya kutosha juu ya kozi zetu ambazo ni za kimkakati ikiwamo kozi ya Uzamili , tuna fanya udahili wa moja kwa moja kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na chuo chetu katika maonesho haya," amesema.

Kaimu huyo amefafanua kuwa NIT wanafanya tafiti mbalimbali kujua mahitaji yaliyopo katika soko la ajira ili kuisaidia serikali katika kutekeleza miradi yake ya kimkakati.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI