Na Asha Mwakyonde, Dar es salaam
UDAHILI wa wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe (MU), umekuwa ukiongezeka ikilinganishwa na mwaka juzi ikiwa ni matokeo ya pamoja yanayofanywa na wafanyakazi wa chuo hicho kwa kuzitangaza programu ambazo zinatoa matokeo chanya kwa Watanzania.
Akizungumza jijini Dar es salaam Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa William Mwegoha katika Maonesho ya 18 Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU),ambayo yalianza Julai 17, na kuhitimishwa leo Julai 22, 2023 kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja yenye kaulimbiu isemayo 'Kukuza Ujuzi Nchini kupitia Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia kwa Uchumi Imara na Shindani', amesema mwaka jana wameweza kudahili wanafuanzi zaidi ya 13735 ikilinganishwa na mwaka juzi ambapo walifanya Udahili wa wanafunzi 13078 huku akisema Udahili huo umekuwa ukiongezeka.
Prof.Mwegoha ameaema hayo ni matokeo ya pamoja wanayoyafanywa na wafanyakazi wa chuo hicho kwa kuzitangaza programu zao nzuri na zinatoa matokeo hayo huku akitolea mfano programu ya Sheria ambayo wanafundisha kwa vitendo.
Ameongeza kuwa chuo hicho wanafunzi wake wanaoongoza kuchukuliwa kwenda kujitolea sehemu mbalimbali baada kumaliza masoma yao ambapo kupitia huko wanapata ajira za kudumu na kwamba viongozi wengi serikalini wamepitia katika Chuo Kikuu Mzumbe.
"Lengo la maonesho haya ni Vyuo kukutana na kukutanisha Umma juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Vyuo hivi na sisi Chuo Kikuu Mzumbe tumekuja kutangaza programu ambazo tunazitoa kuanzia ngazi ya chini hadi hatua ya juu kabisa," ameongeza.
Nashukuru tumeweza kupata watu wengi waliotembelea katika banda hili na kuja kuona programu zetu," ameeleza Prof.Mwegoha.
Prof.Mwegoha amewataka wanafunzi kufanya udahili wa kujiunga na chuo hicho kabla dirisha la kwanza halijafungwa na TCU na kwamba Chuo hicho kinaendelea kufanya udahili wa wanafunzi hadi ifikapo Oktoba mwaka huu.
Ameongeza kuwa programu zinazotolewa na Chuo Kikuu Mzumbe ni nzuri na zinamanufaa makubwa kwa Watanzania.
0 Comments