Na Asha Mwakyonde, Dar es salaam
CHUO Kikuu cha Dodoma (UDOM), kimeshiriki kikamilifu katika mradi wa Jenga Kesho iliyo Bora (BBT), ambao ni maalumu kwa vijana lengo likiwa ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwenye miradi mikubwa ya kimaendeleo na ya kimkakati.
Mradi huo wa BBT ulizinduliwa na Rais Dk. Samia Machi,2023 ambapo vijana 812 walichaguliwa kujiunga.
Akizungumza jijini Dar es salaam jijini katika banda la chuo hicho Naibu Makamu Mkuu wa UDOM (Mipango, Fedha na Utawala), Profesa Wineaster Anderson, katika Maonesho ya 18 Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU),ambayo yalianza Julai 17, na kuhitimishwa leo Julai 22, 2023 kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja yenye kaulimbiu isemayo 'Kukuza Ujuzi Nchini kupitia Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia kwa Uchumi Imara na Shindani', amesema wapo baadhi ya wataalam walihusika kutoa ushauri kuhusu mradi wa BBT.
Prof. Wineaster ameeleza kuwa chuo hicho kinatatua changamoto zinazoikabili jamii kwa
kinazalisha wataalam, kufanya tafiti na kuibua bunifu mbalimbali.
"Chuo kinaendelea kushirikiana na Serikali ili kufanikisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo inafanikiwa ameeleza Prof. Wineaster.
Akizungumzia uwepo wao Katika maonesho hayo amesema wameyatumia kutoa elimu kwa Watanzania na kueleza fursa zinazopatikana ikiwa ni pamoja na machapisho mbalimbali.
Chuo hicho kina wanafunzi zaidi ya 30,000 na kinafanya vizuri katika maeneo mbalimbali yakiwamo katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA),pamoja na kushinda mashindano ya kitaifa na kimataifa.
0 Comments