MIAKA 25 JELA KWA KOSA LA SHAMBULIO LA AIBU


Zanzibar 

Mahkama ya Mkoa wa Vuga, leo tarehe 22/09/2023 imemhukumu mshtakiwa SAID MOHAMED ABDALLAH (29) Mshirazi na mkazi wa Mbuzini Zanzibar kutumikia kifungo cha miaka 25 Chuo cha Mafunzo (jela) na kulipa fidia ya Shilingi 1,000,000 kwa makosa la Shambulio la Aibu.

Awali mshtakiwa huyo alishtakiwa kwa kosa la shambulio la aibu kwa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka kumi (10) ambapo mshtakiwa mnamo tarehe 08/08/2019 majira ya saa 5:00 asubuhi huko Mbuzini Wilaya ya Magharibi A" Mkoa wa Mjini Magharibi alimpandisha nguo kisha kumsugulia uume sehemu za siri za mtoto huyo jambo ambalo ni kosa kinyume na kifungu namba 114(1) Cha sheria ya adhabu namba 6/2018 Sheria ya Zanzibar.

Akisoma maelezo ya hukumu hiyo, Hakimu Mhe. Luciano Nyange amesema Mahkama imejiridhisha na ushahidi uliotolewa mbele ya mahkama hiyo ambao haukuwa na chembe ya shaka ambapo umemtia hatiani mtuhumiwa kwa kosa hilo.

Jumla ya mashahidi watano (05) walitoa ushahidi mahakamani hapo.

Kesi hiyo ilifunguliwa Mahkamani tarehe 12/11/2019 ambapo ilipewa kesi namba 380/2019

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI