Na mwandishi wetu
Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Songea Vijijini washauriwa kuendelea kuimarisha miradi ya uchumi ambayo itasaidia katika kuchechemua uhai wa miradi ya maendeleo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika ngazi ya kata.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Jenista Mhagama na Mbunge Peramiho, wakati wa Maadhimisho ya wiki ya UWT Wilaya ya Songea yaliyofanyika katika Kata ya Maposeni.
“Nimetoa kinu cha kupukuchulia Mahindi, kwa ajili ya (UWT) wilaya Songea; kama moja ya kitega uchumi kingine, naomba Kamati ya Uchumi kutumia miradi hii kuimaisha Ofisi ya (UWT) katika kata zote,” alieleza.
Aidha katika harambee ya ujenzi wa nyumba ya Mtumishi wa (UWT) Wilaya ya Songea Vijijini, Waziri ametoa mabati ya ujenzi wa jengo zima na kiasi cha shilingi millioni moja kwa ajili ya gharama za ujenzi wa fundi,"alisema
Amefafanua kwamba lengo la kuanzishwa kwa UWT ni kumkomboa mwanamke.
“Mhe. Rais anajua mahitaji ya wanawake ya Msingi na mahitaji hayo pamoja na kuwasaidia wanawake yanawafaa pia na wanaume. Hakuna Rais amejenga vituo vingi vya Afya na zahanati nyingi kama Rais, Dkt. Samia Suluhu Hasssan,” amebainisha
Awali akizungumza wakati wa kukata keki ya Harambe, Mwenyekiti wa wa Kamati ya Uchumi ya Wilaya (UWT) Bi, Clementina Komba, ameomba wanawake kuamka na kupeana moyo katika kufanya kazi ili kuinua uchumi wa wanawake.
“Kamati ya uchumi tupo tayari kupita na kuelimishana kata kwa kata ili kujenga uelewa katika eneo ulilopo ni kitu gani ufanye ili kuimarisa uchumi,” alisema.
Maadhimisho hayo yameenda sambamba na zoezi la uchangiaji damu; kufanya usafi wa mazingira kugawa taulo za kike kwa wanafunzi wa sekondari, kufungua daftari la UWT na usajili, na elimu ya kupinga ukatili na elimu ya uchumi.
0 Comments