UWT DODOMA WAMPA DK. TULIA MAUA YAKE


Na Asha Mwakyonde, Dodoma

UMOJA wa Wanawake Tanzania (UWT),mkaoni Dodoma ni miongoni mwa watu waliojitokeza kumpakea  Spika wa Bunge la Tanzania Dk. Tulia Ackson baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU),katika uchaguzi uluofanyika nchini Angola.

Dk. Tulia alichaguliwa kuwa Rais wa 31 wa  IPU baada ya kushinda wagombea kutoka nchi za Senegal Adjidiarra Kanoute  aliyepata kura 59, Catherine Hara wa Malawi kura 61 na Marwa Hagi kutoka Somalia aliyepata kura 11.

Akizungumza jijini hapa leo Oktoba 30,2023, katika uwanja wa ndege wakati wa mapokezi ya Dk. Tulia Rais wa IPU, Mwenyekiti wa UWT MKoa wa Dodoma Neema Majule amesema kuwa wamefurahishwa na ushindi huo na kwamba wameenda kumpatia maua yake uwanjani hapo.


Mwenyekiti huyo ameeleza kuwa nafasi hiyo aliyoipata Dk. Tulia inaonesha wanawake wanaweza huku akisema ushindi huo ni nguvu ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumuruhusu kwenda kugombea.

"Ni furaha yangu kubwa leo tumekuja uwanjani hapa na wanawake wenzangu wa UWT Mkoa wa Dodoma kwa wingi wetu kumpakea na kumpongeza Spika kwa ushindi mkubwa wa IPU," amesema Neema.

Ameongeza  matarajio yao ni makubwa katika nafasi aliyoshinda Dk. Tulia kwa uwakilishi wa nchi  na duniani na kwamba Tanzania imezidi kujulikana kutokana kwa kuwa  Rais  wake ni mwanamke pamoja na Filamu ya' Royal Tour'.

 "Ushindi wa Dk. Tulia ni wa wanawake wote nchini  hii ni kutokana na mazingira mazuri yaliyowekwa na Rais Dk. Samia ya kuwaamini wanawake katika masuala ya uongozi, " amesema.


Naye Katibu wa UWT , Mkoa wa Dodoma, Getrude Izengo, amesema kuwa wameona fahari kwa heshima hiyo kubwa ambayo wameipata kupitia nafasi aliyoshinda Dk. Tulia.

" Wanawake wa UWT na wanawake wengine tumekuja kumpakea Rais wa IPU kwa heshima aliyotuletea  sisi wanawake na Taifa kwa ujumla," amesema.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI