ASIMAMISHWA KAZI KWA KULEWA POMBE


Na Mwandishi wetu, Dodoma 

MTENDAJI wa kata ya Manchali Wilaya ya Chamwino, Waitara Wambura amesimamishwa kazi kwa kukiuka maadili ya kazi na kulewa pombe katika masaa ya muda wa kazi ikiwamo ni pamoja na kuonesha utovu wa nidhamu.

Akimsimamisha kazi mtendaji huyo Februari 21,2024 jijini Dodoma  Mkuu wa Mkoa Rosemary Senyamule akiwa katika muendelezo wa ziara zake za kikazi katika wilaya hiyo ikiwamo 
kukagua Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Mkoa ,Ujenzi wa uzio wa Jengo la ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino, Ujenzi wa Zahanati ya Wilunze ,eneo la maadhimisho ya siku ya wanawake pamoja na kufanya mkutano wa hadhara na Wananchi wa Kata ya Manchali.

Rosemary amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri  hiyo kufanya uchunguzi wa kina juu ya utendaji kazi wa mtendaji huyo.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa ameagiza Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kukamilisha ujenzi wa uzio wa ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kabla ya Machi 30, mwaka huu.

Rosemary ametoa agizo hilo ni kutokana na kudorola kwa mradi huo zaidi ya miezi 8 tangu ulipotakiwa kukamilika mwezi  Julai 2023.

Ameongeza kuwa picha ya Chamwino kwa Sasa siyo nzuri ambapo Mkoa una Halmashauri nane na katika Halmashauri hiyo  kila miradi unaoenda  lazima zijitokeze changamoto.

 "Tunapokea malalamiko yenu mengi hasa suala la malipo Kwa wakandarasi wanaojenga miradi yenu, Rais anatoa fedha zote ila nyie mnachelewesha kuwalipa na hiyo ndio sababu inachangia mradi kutokukamilika kwa wakati," amesema.

Kwa upande wake kaimu  Mkuu wa wilaya ya Chamwino Godwin Gondwe ameahidi kusimamia bega Kwa bega miradi inayotekelezwa katika wilaya hiyo na kukamilika Kwa ubora na muda uliopangwa.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI