TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA MWAKA WA WAKE WA MARAIS WA AFRIKA


Dubai 

TAASISI ya Merck Foundation ya Dubai kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajia kuandaa Mkutano wa Mwaka wa Wake wa Marais wa Afrika ambao wanatekeleza miradi mbalimbali ya kuwawezesha wanawake katika nchi zao chini ya ufadhili wa Merck Foundation. 

Kikao cha kwanza cha maandalizi ya Mkutano huo kimefanyika tarehe 20 na 21 Februari,  2024 Dubai Makao Mkuu ya Merck Foundation.

Tanzania imechaguliwa kufanyika kwa Mkutano huo muhimu kutokana na juhudi  za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Utawala Bora na kuwezesha Wanawake katika nyanja zote za maendeleo. 

Pamoja na kunufaika na fursa mbalimbali za ufadhili wa miradi ya Merck Foundation, Tanzania itaendelea kujitangaza Duniani kwa kuwa Mkutano huo utahudhuriwa moja kwa moja na washiriki zaidi ya 500 kufuatiliwa na zaidi ya watu milioni 5 kwa njia ya mtandao kutoka mataifa 70 yanayonufaika na Merck Foundation. 

Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akiwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii na Watoto Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Riziki Pembe Juma pamoja na Katibu Mkuu Dkt. Seif Shekalaghe kwa uratibu  wa Ubalozi wa Tanzania Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI