VYOMBO VYA HABARI VYA TAHADHARISHWA KURIPOTI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

Na Asha Mwakyonde, Dodoma 

NAIBU Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Mathew Kundo amevitaka vyombo kuwa mstari wa mbele kwa kuzingatia Maadili na kanuni za utoaji habari kwa jamii kwa maslahi ya Taifa hasa katika  kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao unatarajiwa kufanyiwa mwaka huu.

Pia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),ameiagiza Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA,kuhakikisha inajitathmini mara kwa mara lengo linikiwa ni kutoa mwelekeo wapi kuna mapungugu na ili yaweze kufanyiwa kazi mapungugufu hayo.

Hayo yameelezwa leo Februari 
13,2024 Jijini hapa wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji Nchini ulioenda sambamba na kilele cha maadhimisho ya siku ya Utangazaji Duniani amesema ni vema vyombo hivyo kufuatilia kwa umakini mafunzo ya kanuni za uchaguzi katika kuelekea uchaguzi Mkuu wa Serikali za Mitaa kwa kuwa vina wajibu wa kutoa taarifa sahihi kwa Wananchi ili uchaguzi Uwe wa amani na haki.



Mkandisi  Kundo amewaasa waandishi wa habari kuhakikisha wanazingatia usawa katika kuripoti matukio ya kampeni za Uchaguzi na matokeo yake bila upendeleo

Aidha Kundo amevitaka vyombo vya habari kuanzisha vipindi vinavyo hamasisha mila na Destiri ya mtanzani ilikuwaelimisha vijana kuhusu tamaduni zao.

"Ni muhimu kila mmoja kuzingatia taaluma na kutimiza majukumu yake kwa weledi hivyo 
vyombo vya habari vina wajibu mkubwa katika Taifa letu," ameeleza.

Kwa upande Wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania( TCRA )Jones Kilimbe ameeleza kuwa 
vyombo vya habari vina jukumu la kutoa elimu kwa wapiga kura na kuhabarisha umma kuhusu mchakato mzima wa kampeni bila upendeleo na kutoa ripoti sahihi za siku ya kupiga kura. 

Naye Mwenyekiti wa wamiliki wa Vyombo vya Habari Nchini( MOAT)Samwel Nyala 
ameiomba Serikali kuangalia suala hilo ikiwa ni pamoja na kuangalia suala la ruzuku kwa Vyombo vya Habari kutokana na kuwepo kwa mdororo wa Uchumi.

Kwa upande wake mdau wa habari kutoka Chama cha watangazaji (NIPA) Amos Ngosha ameiomba Serikali kuanza kutoa ruzuku kwa vyombo vya habari ili viweze kujiendesha.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI