HOSPITALI ZA RUFAA KUTOA HUDUMA SAA 24, WANAOTUMIA NHIF KUTIBIWA


Na Asha Mwakyonde,Dodoma

HOSPITALI za Rufaa za Mikoa zimejipanga kuwahudumia wagonjwa wote wanaotumia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), fedha taslimu pamoja na wale wa msamaha ikiwa ni pamoja na kutoa huduma saa 24.

Akizungumza jijini Dodoma leo  Machi 01,2024  Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dk. Ibenzi Ernest ambaye pia ni Mwenyekiti  Mfawidhi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa Tanzania Bara amesema kuwa 
kitita cha kutolea huduma hasa kwa wagonjwa wanaotumia bima ya NHIF, kimeboreshwa ambapo dawa nyingi zimeingizwa ambazo hazikuwepo awali

Dk. Ibenzi amefafanua kuwa Rais Dk. Samia  Suluhu Hassan amefanya uwekezaji  katika kuongeza wataalamu wa afya, vifaa tiba, dawa pamoja na vitendanishi katika Hospitali za mikoa ambazo zimeimarika kwa utoaji wa huduma kwa wagonjwa.


Amesema jana walikuwa na kikao cha waganga wafawidhi kutoka mikoa 28 nchini ambapo walikubaliana kuanza kutoa huduma kwa wagonjwa kuanzia saa moja na nusu asubuhi hadi wagonjwa hao watakapomalizika tofauti na awali walivyokuwa wakitoka kazini saa tisa na nusu jioni.

Mganga Mfawidhi huyo ameeleza kuwa lengo ni kuwahudumia wangonjwa wao kwa wakati bila kusababisha ukosefu wa huduma katika maeneo yao ya kazi.

"Tuinashukuru Wizara ya afya kwa kuendelea kuzisimamia hospitali zetu za Rufaa za mikoa kuziwezesha kwa kutuletea wataalam wa kutosha hivi karibuni imeajiri wataalam hawa lengo kubwa ni kuziba mapengo yaliyowepo, serikali ya awamu ya sita imewekeza kwenye sekta ya afya na wizara nayo imepanga mipango yake ili kuwezeaha kupata wataalam," ameeleza.

Aidha amemshukuru  Rais Dk.Samia  kwa kazi kubwa ambayo anaendelea kuifanya katika nchi na kwamba wapo  katika mwendelezo wa uboreshaji wa huduma za afya hapa nchini na  wanajua uwekezaji makubwa katika sekta ya afya uliofanywa na Rais huyo wa awamu ya sita.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU