DK. BITEKO KUWA MGENI RASMI KESHO MKUTANO WA 13 TEF

Na Asha Mwakyonde,Dodoma 

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk. Doto Biteko anatarajiwa kuwa mgeni rasmi leo katika mkutano 13 wa kitaaluma wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF),unaolenga kujadili mada mahsusi na kwamba Kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Nafasi ya vyombo vya habari katika matumizi ya gesi kwa ajili ya kulinda misitu', ambao  utashirikisha wahariri 150 kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Akizungumza leo Aprili 28,2024 jijini hapa na waandishi wa habari Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TEF, ambaye pia ni mhariri wa gazeti la FAMA Neville Meena alisema kuwa mkutano huo utafanyika jijini hapa kwa muda wa siku mbili.

Mjumbe huyo amesema kauli mbiu hiyo inayoongoza katika mkutano huo itatumika kama mada kuu 

 na kwamba kutakuwa na watoa mada mbalimbali za kitaaluma ikiwamo ya wanawake na uongozi katika vyumba vya habari, nafasi zao wajibu wao pamoja na uzingatiaji wa taaluma.

"Tupo Dodoma tunajambo letu la kitaaluma ambalo litafanyika Aprili 29 na 30 tutakuwa na mkutano kitaaluma wa 13, namada nyingine itakuwa ni kuhusu uchaguzi kama tunavyofahamu mwaka huu tutakuwa na uchaguzi wa serikali za mitaa na mwakani tukijaaliwa tutakuwa na uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani" amesema Meena.

Amesema watakuwa na mada hiyo kwa kuwa wanahusika na kuandika habari ikiwa ni pamoja na kuelekeza akili zao katika suala la uchaguzi huku akisema mada nyingine ni jinsi gani ya ufanyaji kazi kwa kuzingatia teknolojia inavyokua katika vyombo vya habari na watakavyokabiliana na Teknolojia ya akili Mnemba.

"Vyombo vyetu vya habari haviwezi kufanya kazi pasipo kuzingatia mabadiliko makubwa ya teknolojia,ule utawala wa magazeti, wa runinga kufikiria kila kitu kwamba bila wao kutanzangaza hakuna kitakachotokea, vyote hivyo vitaendelea kuwepo lakini tuzingatie teknolojia imekua kuna mitandao ya kijamii inafanya kazi," amesema.

Meena amesema ni jinsi gani kwamba vyombo vya habari vinaweza kufanya kazi kwa kuunganisha utaalumu uliopo ndani ya vyombo hivyo na mabadiliko ya teknolojia.

Naye mjumbe wa kamati hiyo Salim said Salim amesema kuwa waandishi wengi wanafanya habari za kiongozi fulani kapanda miti huku akisema wanandishi hao hawafuatilii maendeleo ya miti hiyo.

Pia amewataka waandishi wa habari kufanya kazi kwa ueledi bila kuegemea upande mmoja na badala yake kuandika zile zinasoigusa kijamii.

Mkutano huo pia unatarajiwa kuhudhuriwa na Waziri wa Habari Mawasoliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI