MBUNGE ULANGA AMEIHOJI SERIKALI UJENZI HOSPITALI MPYA YA ULANGA


 Na Asha Mwakyonde, Dodoma 

SERIKALI imetenga shilingi bilioni 27.9 za ukarabati wa hospitali kongwe 31 zilizobaki ikiwemo Hospitali ya Wilaya ya Ulanga ambayo imepokea shilingi milioni 900 na ujenzi na ukarabati wa majengo mbalimbali unaendelea. 

Akijibu swali la mbunge wa Ulanga Salm Hasham bungeni leo Aprili 29, jijini Dodoma katika swali lake la msingi ambapo amehoji ni lini Serikali itajenga Hospitali mpya ya Wilaya ya Ulanga? Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dk. Festo Dugange (OR TAMISEMI), amesema 

Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga ilianza kutoa huduma mwaka 1905 kama kituo cha afya na baadae kupandishwa hadhi na kuwa hospitali.

Ameongeza kuwa Hospitali hii ni miongoni mwa hospitali kongwe 50 ambazo Serikali ilizifanyia tathmini kwa ajili ya ukarabati mkubwa.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU