BALOZI DK.CHANA: WIZARA KUFANYA MAPITIO MFUMO WA HAKI JINAI, MASHAURI 196,592 YAMESHUGHULIKIWA


Na Asha Mwakyonde, Dodoma 

WIZARA ya Katiba na Sheria imeesema imeendelea kusimamia na kuratibu utekelezaji wa mipango inayolenga kufanikisha jukumu la 

kuendelea kuimarisha mifumo ya utoaji haki ili haki hiyo ipatikane na kuweka mazingira yanayohakikisha usawa kwa wote na kwa wakati kwa kushughulikia masuala manne muhimu.

Akiwasilisha bungeni jijini hapa leo Aprili 29,2024,Waziri wa Wizara hiyo Balozi Dk. Pindi chana hutuba yake ya Mipango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2024/ 2025 ameyataja mambo hayo muhimu kuwa ni kufanya mapitio ya mfumo wa Haki Jinai na kuandaa mpango wa marekebisho ya sheria ambazo zinatoa mianya ya ama kuchelewesha upatikanaji wa haki au ukandamizaji katika kupatikana haki.

Balozi Dk Chana amesema mengine ni kuongeza kasi ya usikilizaji wa mashauri yaliyosajiliwa mahakamani ili kupunguza na hatimaye kumaliza kabisa mrundikano wa mashauri Mahakamani, kuendelea kutekeleza Mpango wa Ujenzi na Ukarabati wa Majengo ya Mahakama katika ngazi mbalimbali na kutekeleza mradi wa maboresho ya mifumo ya Huduma za Mahakama kwa njia za kielektroniki.

Akizungumzia kuhusu mpango wa kupunguza mrundikano wa mashauri mahakamani, katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024 ameeleza kuwa Mahakama imeshughulikia jumla ya mashauri 196,592.

" Kati ya mashauri haya, mashauri 133,82 yamesikilizwa na kuhitimishwa na mashauri 62,769 yaliyobaki yanaendelea kusikilizwa," amesema Balozi Dk chana.

Balozi Dk. chana ameeleza katika mashauri yanayoendelea kusikilizwa, mashauri ya umri mrefu ni 2,087 sawa na asilimia 3 ya mashauri yote yaliyobaki Mahakamani. 

Ameongeza kuwa utekelezaji wa Mpango wa Ujenzi naUkarabati wa Majengo ya Mahakama katika ngazi mbalimbali, hadi kufikia Aprili, 2024, miradi ya ujenzi iliyokamilishwa ni Mahakama za Wilaya ya Ulanga, Kwimba na Liwale; Ukarabati wa jengo la Mahakama ya Wilaya ya Maswa.


Balozi huyo amesema ujenzi wa Majengo ya Mahakama za Mwanzo Usevya Mlele, Nyakibimbili Bukoba, Mahenge Kilolo, Newala Mjini, Madale Dar es Salaam, Kinesi Rorya na Luilo Ludewa. 

"Majengo ya Mahakam yanayoendelea ama kujengwa au kukarabatiwa ni kama Ujenzi wa Vituo Jumuishi vya Utoaji Haki sita vya Katavi, Songea Ruvuma, Songwe, Njombe, Simiyu na Geita," ameeleza Balozi Dk. chana.

Waziri huyo amesema ujenzi wa majengo ya Mahakama za Mwanzo tatu ambazo ni Ilangala Ukerewe, Mbalizi Mbeya na Machame Kilimanjaro.

Amesema kuendelea kwa ujenzi wa majengo ya Mahakama za Wilaya sita ambazo ni Kibiti Pwani, Nachingwea Lindi, Simanjiro Manyara, Hanang Manyara, Mbulu Manyara na Tunduru Ruvuma pamoja na Ujenzi wa jengo la Mahakama ya Wilaya ya Korogwe ambapoutekelezaji wake umefikia asilimia 61.

Waziri Balozi Dk. chana ameeleza kuwa Ujenzi wa Jengo la Mahakama ya Wilaya Ubungo ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 98, Ukarabati wa jengo la zamani la Mahakama Kuu Dodoma ambapo ukarabati umefikia asilimia 49.

Amesema Ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Mahakama ambapo hadi sasaumefikia asilimia 97.3, ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Kabanga-Ngara unaendelea na upo asilimia 97, ujenzi wa nyumba 48 za Majaji eneo la Iyumbu Dodoma ambapo ujenzi umefikia asilimia 98 na kuendelea na ujenzi wa nyumba ya Jaji Mkuu, jijini Dodoma ambapo ujenzi umefikia asilimia 53.

" Kuimarisha mifumo ya utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala kwa kuanzisha na kuendesha Kituo cha Kimataifa cha Utatuzi wa Migogoro na katika mwaka 2023/2024, Serikali imesajili jumla ya watoa huduma 46 walioomba kuthibitishwa kama Watoa Huduma za Utatuzi wa Migogoro kwa njia mbadala, ambapo Waendesha Maridhiano 3, Watoa Huduma za Majadiliano 3, Wapatanishi 13 na Wasuluhishi 27," amesema.

Waziri huyo amefafanua kuwa hadi Aprili, 2024 wapo Watatuzi wa Migogoro kwa njia Mbadala 576, kati ya hao, Waendesha Maridhiano 38, Watoa Huduma za Majadiliano 60, Wapatanishi 185 na Wasuluhishi 293.

Amesema Serikali inaendelea na taratibu za kuanzisha Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi Tanzania (Tanzania International Arbitration Centre), Taasisi hiyo itakuwa na Kituo Dar es Salaam ambapo tayari jengo kwa ajili ya kuanzisha Kituo hicho limepatikana.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI