Kisarawe, Pwani
VIONGOZI wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Taifa, wakiongozwa na Mwenyekiti wetu kipenzi, Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), wamefanya ziara ya mafunzo katika Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)—Kiwanda cha Nishati Safi ya Rafiki Briquettes, kilichopo Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani, leo tarehe 22 Julai 2026.
Katika ziara hiyo, viongozi walipata fursa ya Kujifunza hatua zote za uchakataji wa makaa ya mawe kuwa Nishati Safi (Rafiki Briquettes), Kushuhudia utendaji wa mashine za kisasa za viwandani na majiko ya Majumbani na Kupata ufafanuzi wa kina kuhusu ubora, usalama, pamoja na fursa za ajira na uwekezaji.
Akizungumza na Menejimenti ya STAMICO, Mwenyekiti wa UWT Taifa ameongeza na kulipongeza Shirika hilo kwa kazi kubwa inayofanyika kutafsiri kwa vitendo maono ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kusukuma mbele ajenda ya nishati safi ya kupikia.
Aidha, UWT imeeleza utayari wake wa kuwa Mawakala Wakuu wa Rafiki Briquettes kwa kushirikiana na STAMICO kuhakikisha elimu inatolewa na bidhaa hiyo inasambazwa katika ofisi zote za UWT Wilaya na Kata nchi nzima.
Ziara hii ni mwendelezo thabiti wa kuunga mkono juhudi za matumizi ya nishati safi na salama kwa afya na mazingira ya Mtanzania.











0 Comments