KASIA YA MALIASILI YAIANGUSHA GST 2-0 SHIMIWI 2026

Na Sixmund Begashe, Moshi

KASI na mbinu ya kipekee ya mchezo wa Kamba imeendelea kuwa silaha ya Timu ya Wanaume ya Wizara ya Maliasili na Utalii katika Michezo ya SHIMIWI 2026, baada ya kuichapa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) mabao 2-0 mjini Moshi, Kilimanjaro.

Timu hiyo inayotumia mtindo unaojulikana kama ‘Kasia’, ilionyesha umahiri na mshikamano mkubwa uwanjani na kufanikiwa kupata mabao hayo ndani ya sekunde tano, hali iliyowashangilia mashabiki waliojitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo.

Ushindi huo umeongeza hamasa kwa mashabiki na wapenzi wa Maliasili Sports Club, ambao wameendelea kuifuatilia timu hiyo kwa karibu katika michuano hiyo inayoendelea mkoani Kilimanjaro.

Baada ya ushindi huo, timu hiyo inatarajiwa kuingia tena uwanjani Septemba 26, 2026, kwa kukutana na timu ya Ikulu Kamba ME katika siku ambayo pia imepangwa kufanyika sherehe rasmi za ufunguzi wa Michezo ya SHIMIWI 2026.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na uwezo wa timu hizo, huku mashabiki wakisubiri kuona namna Maliasili Sports Club itakavyotumia mtindo wake wa ‘Kasia’ dhidi ya Ikulu Kamba ME.





Post a Comment

0 Comments

 DK. HOMERA: AWATAKA WATANZANIA KUWA NA SUBIRA KUHUSU MABADILIKO YA KATIBA