MKARUDI NA USHINDI- ADA- MLINGA


 Na Sixmund Begashe, Dodoma

TIMU za Maliasili Sports Club zimetakiwa kuhakikisha zinacheza kwa nguvu, juhudi na maarifa michezo yote katika Michuano ya SHIMIWI 2026 ili kuhakikisha zinaipatia Wizara ya Maliasili na Utalii ushindi wa hali ya juu. 

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo Bi. Violeth Mlinga wakati akiiga timu hiyo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi kabla ya kuanza safari yao kuelekea Moshi, Mkoani Kilimanjaro. 

Mlinga amesisitiza kuwa, Wizara hiyo imeiamini Club hiyo hivyo wachezaji wana wajibu wa kuzingatia weledi na taratibu zote za Utumishi wa Umma ili kulinda taswira ya Wizara hiyo ili kuibuka na matokeo chanya ambayo ni ushindi kwa timu zote. 

Ameongeza kuwa, ushiriki wa Wizara hiyo katika michuano hayo ni sehemu ya kuongeza wigo si tu wa kutangaza shughuli za Wizara bali kujenga pia uhusiano mwema wa kiutumishi na Wizara zingine kwa maslahi mapana ya taifa kwa ujumla. 


Naye Mkwenyekiti wa Club hiyo Bw. Elia Mtalemwa, amesema Club hiyo imejiandaa vyema na kuwa lengo kuu ni kurudi na ushindi katika michezo yote kama walivyoelekezwa. 

Pamoja na kuushukuru uongozi wa Wizara kwa mchango mkubwa katika maandalizi na ushiriki wa Club hiyo, amesema timu zote zimejiandaa vyema na kuwa lengo lao kuu ni ushindi kwenye michezo yote. 

Maliasili Sports Club, inaelekea Moshi Mkoani Kilimanjaro kuungana na Wizara zingine kuoneshana ubabe katika Michuano ya SHIMIWI itakayoanza hivi karibuni.






Post a Comment

0 Comments

TECHNOLOJIA YA MATUMIZI YA MIZINGA YA NYUKI YA PLASTIKI YAZINDULIWA MEATU