MBUNGE SANGU AIHOJI SERIKALI UJENZI BARABARA YA CHOMBE

Na Asha Mwakyonde, Dodoma 

MBUNGE wa Kwela, Deus Sangu leo bungeni Aprili 30,2024 jijini Dodoma katika swali lake la msingi ameihoji serikali ni lini ahadi ya Viongozi ya Ujenzi wa Barabara ya Chombe Kaoze Kwela itatekelezwa? 

Akijibu swali hilo Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Zainabu Katimba amesema Serikali inatambua umuhimu wa ujenzi wa barabara ya Chombe hadi Kaoze Kwela yenye urefu wa kilomita 15.

Naibu Waziri huyo ameeleza kuwa 
barabara hiyo inaunganisha vijiji vya Kaoze, Kiandaigonda na Chombe ambayo ipo sambamba na milima ya Lyambalyamfipa imeathiriwa na maji ya mvua. 

"Serikali kupitia Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), imekamilisha usanifu wa madaraja na barabara na kubaini gharama ya shilingi bilioni 2.3," amesema Katimba.

Ameongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2024/25, Serikali imetenga shilingi milioni 500 kupitia fedha za tozo ya mafuta kwa ajili ya kujenga kipande cha barabara kati ya kijiji cha Kaoze na Kiandaigonda.

Naibu Waziri huyo amesema Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya barabara hii ili kukamilisha ujenzi wa kipande cha kutoka kijiji cha Kiandaigonda hadi Chombe.

Mbunge huyo akiuliza maswali mawili ya nyongeza alisema kuwa 
barabara ya Chombe -Kiandaigonda hadi Kaoze ni barabara ambayo imeandikiwa kuomba maombi maalumu kwa miaka miwili mfululuzo ya shilingi bilioni 2.4 hivyo ametaka kujua serikali ina mpango gani wa kupitia maombi hayo ya kuweza kupeleka fedha kwa ajili ya barabara hiyo ?

Katika swali lake la pili amesema daraja linalounganisha Kijiji cha Ilembo na Makao Makuu ya Kata ya Mpuyu imeharibiwa na kwamba wamepeleka maombi ya bilioni 1.35 je serikali ina mpango gani wa kuleta fedha hizo?

Akijibu maswali hayo Naibu Waziri Katimba amesema Serikali inatambu uhitaji huo na maombi ya dharura tayari Naibu waziri ofisi ya Rais TAMISEMI aliyepita alienda kufanya ziara katika eneo hilo pamoja na mtendaji Mkuu wa TARURA na kwamba tayari serikali inatambua umuhimu na ipo kwenye mchakato hivyo ombi limepokelewa na wanalifanyia kazi

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU