Msumbiji
NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew amewasili nchini Msumbiji leo Aprili 24, 2024 kwaajili ya kushiriki katika Mkutano wa 11 wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa Kamisheni ya bonde la mto Zambezi.
Pamoja na masuala mengine, mkutano huo utajadili kuhusu utekelezaji wa Mpango Kazi wa ZAMCOM mwaka 2023/2024 na kupitisha Mpango Kazi na Bajeti ya Kamisheni ya Bonde la Mto Zambezi katika mwaka 2024/2025;
Pia, utajadili masuala ya utafutaji fedha kwa ajili ya Programu ya Maendeleo Jumuishi na Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi katika Bonde la Mto Zambezi (Programme for Integrated Development and Adaptation to Climate Change in the Zambezi Watercourse – PIDACC Zambezi) ambayo Tanzania itashiriki kuitekeleza.
Katika safari hiyo ya Nchini Msumbiji Mhe. Kundo ameongozana na Mkurugenzi Rasilimali za Maji Dkt George Lugomela, Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali za Maji Bw. Robert Sunday pamoja na Mkurugenzi wa Bonde la Ziwa Nyasa Mhandis Elice Engelbert.
Mkutano huo utafanyika kuanzia tarehe 25 hadi 26 Aprili 2024 kwenye Mji wa Tete uliopo Nchini Msumbiji.
0 Comments