EWURA YAANZA KUSAJILI VILAINISHI VILIVYOKUWA VIKIAGIZWA NJE YA NCHI


Na Asha Mwakyonde, Dodoma 

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imeanza kusajili vilainishi vinavyozalishwa na kuagizwa kutoka nje ya nchi kwa lengo la kuhakikisha vilainishi vyenye ubora uliothibitishwa na taasisi za ndani na kimataifa vinatumika nchini.

Hayo yamesemwa leo Aprili 24, 2024 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk.Doto Biteko wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2024/25 amesema Mamlaka hiyo inaendelea kutoa elimu kwa watumiaji kununua bidhaa hizo kutoka kwa wauzaji waliothibitishwa.

Amesema serikali kupitia EWURA ilowndelea na jukumu la kusimamia na kukagua soko la ndani la mafuta ili kuhakikisha mafuta yanayouzwa nchini yana viwango stahiki vya vinasaba kwa lengo la kudhibiti ubora na kuimarisha mapato ya serikali kupitia kodi.

Dk. Biteko ameongeza kuwa Mamlaka hiyo ilipima mafuta kwenye vituo 307 ambapo vituo 299 sawa na asilimia 97.39 vilifaulu kwa kuwa na kiwango stahiki vinasaba.

Akizungumzia bidhaa za mafuta ya petroli Dk. Biteko ameeleza kuwa Serikali imeendelea na Usimamizi wa ubora wa vituo vya mafuta ili kuimarisha upatikanaji, usalama na ubora wa bidhaa za mafuta kwa watumiaji katika maeneo yote nchini.

" Serikali imeendelea kusimamia mazingira chanya ya uwekezaji ujenzi wa vituo vya mafuta yenye ubora ambapo hadi kufikia Machi 2024 jumla ya vituo hivyo 2,522 vilivyopo mjini na vijijini vilikidhi vigezo vya ubora na usalama na kupewa leseni ikilonganishwa na vituo vya 2,297 katika kipindi cha hicho mwaka 2022/ 2023 sawa na ongezeko la asilimia ,9.80.0, kati ya vituo hivyo vituo 434 vimejengwa katika maeneo ya vijijini kwa kipindi hicho sawa na ongezeko la asilimia 51. 22 ," amesema.

Ameongeza kuwa katika kipindi cha Julai 2023 hadi Machi Mamlaka hiyo 2024 ilitoa leseni, vibali kuboresha kanuni na kusimamia ubora wa bidhaa za mafuta ambapo ilitoa leseni 34 kwa kampuni za mafuta (Whole Salers), kwa ajili ya kuangiza na kuuza mafuta hayo kwa jumla na leseni 30 zilitolewa kwa kampuni mpya.

Dk. Biteko amesema EWURA ilitoa leseni mpya 4 kwa kampuni za kuangiza na kuuza gesi itokanayo na petroli (LPG), kwa jumla (LPG Whole Salers) na kwamba Mamlaka hiyo ilitoa pia leseni 27 kwa mawakala wa kusambaza LPG ( LPG Distributors).

"Kati ya leseni hizi leseni 26 zimetolewa kwa wakala wapya leseni saba kwa kampuni zenye miundombinu binafisi ya kuhifadhi na kujaza mafuta ( Consumer installation facilities), kati ya hizi leseni sita zilitolewa kwa kampuni mpya," ameeleza.

Ameongeza kuwa Mamlaka hiyo pia ilitoa leseni mpya moja ya ghala la kuhifadhia mafuta ( Petroleum storage), leseni moja ya uwakala wa condensate, vibali vya ujenzi ( construction approvals), 237 ambapo vibali 233 vilikuwa kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya mafuta, kimoja kwa kwa ajili ya miundombinu ya kuhifadhia LPG, viwili kwa ajili ya matumizi ya binafisi ( Consumer installations), na kimoja kwa ajili ya ghala la kuhifadhia mafuta.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI