MHANDISI STELLA AZIOMBA TAASISI, VYUO VIKUU KUONGEZA UBUNIFU VYANZO VYA MAPATO

Na Asha Mwakyonde,Dodoma 

MBUNGE wa Nyasa Mhandisi Stella Manyanya ameziomba taasisi na vyuo vikuu ambavyo vinafanya tafiti mbalimbali viongeze jitihada katika kubuni vyanzo vya mapato ili wanapoenda kwenye maeneo hayo ya kuimarisha, kuboresha suala la fedha lisiwe ni tatizo.

Haya ameyasema leo Mei 8, 2924 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika mwaka wa fedha 2024/2025 amesema vyuo vimekuwa vikibuni mambo nzuri ya kuweza kuisaidia nchi na kwamba suala la kuviwezesha fedha limekuwa ni mdogo.

"Nashauri vyuo hivi viweze kusaidiwa vipewa fedha za kutosha, vijengewe maabara za kutosha, viwanda vya kujifunzia vya kutosha ili mwanafunzi anapohitimu awe amekomaa na aweze kwenda kuonesha kwa vitendo kazi zake kwenye maeneo, hata mwajiri atakuwa na furaha kumuajiri," ameeleza.

Aidha mbunge huyo amesema kuwa anapenda kuona katika mabadiliko wanayoenda nayo shule za amali , ufundi stadi zinawasaidia katika kulitoa Taifa kuondokana na ukosefu wa ajira.

"Sasa nataka nijue tumeshasema tutajenga shule za kutosha zaidi ya 100 kwenye maeneo tumejipanga vipi kwa sababu naogopa mwaka 2016/2017 nilitembelea shule ya ufundi Mtwara nikakuta karakana zake zinatumika kwa ajili ya mfanyabiashara mmoja wa ufundi na magari yake pale hakuna mwanafunzi anayechukua hii fani, nikaenda Ifunda nikakuta mambo ni hivyo hivyo, nilivyoenda Bwiro nikakuta mfanyabiashara nae kapewa karakana anaitumia kwa mambo yake," amesema

Aidha mbunge huyo amesema kuwa anapenda kuona katika mabadiliko wanayoenda nayo shule za amali , ufundi stadi zinawasaidia katika kulitoa Taifa kuondokana na ukosefu wa ajira.

"Sasa nataka nijue tumeshasema tutajenga shule za kutosha zaidi ya 100 kwenye maeneo tumejipanga vipi kwa sababu naogopa mwaka 2016/2017 nilitembelea shule ya ufundi Mtwara nikakuta karakana zake zinatumika kwa ajili ya mfanyabiashara mmoja wa ufundi na magari yake pale hakuna mwanafunzi anayechukua hii fani, nikaenda Ifunda nikakuta mambo ni hivyo hivyo, nilivyoenda Bwiro nikakuta mfanyabiashara nae kapewa karakana anaitumia kwa mambo yake," amesema

Mhandisi Manyanya amefafanua kuwa wanafunzi wawili au watatu wanaenda kujifunza wanavyo takana kwamba hali hiyo imeenda hadi chuo cha walimu kilichokuwa pale Mkwawa kilichokuwa kinafundisha masuala ya ufundi ambapo kinafundisha mambo tofauti.

"Hofu yangu ni kwamba tunaenda kuanzisha shule nyingi ambazo zinahitaji vifaa vingi vya ufundi halafu tusijiweke na kusema tayari tumeshaanza kwa sababu haya mafunzo ya ufundi hayana uongo lazima ufanye lile ambalo linafanana na kumuwezesha huyu mwanafunzi kufahamu inavyotakiwa," amesema.

Mbunge huyo ameeleza kuwa pamoja na juhudi wanazozifanya anaomba wasiwe waoga wa kufanya maamuzi ya kuzisaidia shule hizo, vyuo vya ufundi.

Amesema kuwa mwaka jana walionao kwamba wale wanafunzi wanaochukuwa diploma za kawaida za ufundi wasaidiwe kupata mikopo ambao ndio wanaowategemea kutoka kwenye vyuo hivyo ambavyo watavianzisha huku akisema waliopata mikopo hiyo ni wachache.

Mhandisi Manyanya amefafanua kuwa kutokana na hali hiyo maamuzi yao wanaenda nayo kwa wogo huku akiomba eneo hilo liangaliwe ili wawawezeshe wanafunzi wengi zaidi kuhitimu wakiwa wamepata fursa za kiufundi vizuri na waweze kwenda kulisaidia Taifa.

Akizungumzia suala la kuimarisha elimu msingi amesema hilo halina ubishi kwa kuwa Wizara hiyo ndio inayosimamia Udhibiti ubora wa elimu huku akisema hilo lazima waendelee kulisisitiza kama ambavyo mitaala ya elimu inavyoonekana haiko sawa.

" Wizara hii imepata wachangiaji ambao wengi wanaonekana kuifahamu vizuri na shughuli zake na wanatoa hoja ambazo kimsingi ndizo zinazoendelea katika maisha yetu ya kawaida," amesema.

Mbunge huyo amesema kuwa walifanya jitihada za kukaa pamoja na kushauriana nini kifanyike ndivyo hivyo na kwamba anatamani suala la wanafunzi wanaotoka katika majimbo ya vijijini ambayo hayana watumishi wa kutosha hususan walimu ifike mahali majibu yapatikane.

Amefafanua kuwa haoni sababu Wizara ya elimu kuwa na furaha kwa kuendelea kutoa mtihani mmoja kwa wanafunzi wote wakati wengine hawana walimu huku akisema hiyo sio kuwatendea haki wanafunzi hao.

"Watufahamishe ni namna gani wanawasaidia hawa wanafunzi hasa waliopo vijijini kwa sababu wanakosa elimu iliyosahihi na bora lakini watakosa nafasi za kuendelea na elimu za juu na inapokuja suala la fursa za ajira watazikosa hivyo unakuta baadhi ya maeneo ambayo yataendelea kuwa duni, masikini wakati mmeshasema elimu ndio msingi wetu wa maendeleo," amesema.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI