RAIS DK. SAMIA APONGEZWA KUONGEZA BAJETI YA KILIMO, WABUNGE WATEMBELEA MABANDA YA KILIMO BUNGENI


Na Asha Mwakyonde,Dodoma

MBUNGE wa viti maalum wa Mkoa Mbeya Sophia mwakagenda amempongeza Rais Dk Samia Suluhu kwa kuongeza bajeti ya kilimo ambapo zaidi ya asilimia 60 ya Taifa ni wakulima na kwamba bajeti hiyo imezungumza utaftaji wa masoko nchi za nje kwaajili ya wakulima hao.

Pia wabunge na viongozi mbalimbali wametembelea mabanda ya maonesho yaliyoandaliwa na wizara ya kilimo yaliyopo katika viwanja vya bunge jijini hapa ambapo wametoa maoni yao kuhusu sekta ya kilimo katika kuelekea kuhitimishwa kwa bajeti ya wizara hiyo kesho.

Akizungumza katika viwanja hivyo leo Mei 2,2024 jijini hapa Mwakagenda amesema kupitia bajeti hiyo fedha hizo zikielekezwa katika maeneo makubwa sekta ya kilimo itakuwa na maendeleo makubwa nchini.

Ameongeza kuwa Waziri wa kilimo Hussein Bashe aliyejitoa katika kilimo huku akisema wabaendelea kumuomba asimamie mazao ya chai, kahawa na kwamba bajeti yake kuongezwa ni lazima Waziri huyo ashuke kule chini kama alivyofanya kwenye bajeti iliyopita.

"Tunaendelea kumuamini katika sekta hii na atafanya vizuri kwa kitendo cha kufuatilia wakulima wa chini, "amesema Mwakagenda .

Naye Elizabeth Bolle Meneja Ununuzi wa Mbolea kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), amempongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuleta Mapinduzi ya kilimo nchini na kwamba dhamira hiyo imedhihirika kutokana na uwekezaji mkubwa wa rasilimali fedha katika sekta ya kilimo. 

" Katika mwaka fedha 2020/2023S erikali ilitenga fedha kwaajili ya kutoa ruzuku ya mbolea kwa wakulima ili kuwapunguzia gharama za kununua mbolea hiii na kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao lengo likiwa ni kuhakikosha usalama wa chakula pamoja na kuchangia katika ukuaji wa pato la Taifa," amesema.

Naye Afisa kilimo Mkuu wa wizara ya kilimo Justa Katunzi ameeleza kuwa kuwa huduma za ugani kwa sensa ya mwaka 2019/20 20 ilionesha wastani wa asilimia 6.9 walikuwa wanapata huduma za ugani.

Amesema kuwa juhudi za Serikali za kuongeza uwekezaji katika kuboresha huduma za jamii ikiwemo kilimo imeongeza upatikanaji wa vitendea kazi kwa maafisa ugani ikiwemo pikipiki ili maafisa kilimo hao waweze kuwafikia wakulima kwa urahisi. 

"Tumenunua vifaa vya kupimia udongo ili wakulima waweze kutumia mbolea kulingana na mahitaji yaliyopo katika udongo wao," amesema.

Ameongeza kuwa wizara hiyo ili nunua vishikwambi ili maafisa ugani waweze kuwasiliana na wakulima kupitia simu zao za mkononi ambapo hata kama hajamfikia mkulima anaweza kutuma ujumbe na kupatiwa ushauri.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI