SERIKALI YAAGIZA MAMLAKA ZA MIKOA KUENDELEA KUCHUKUA TAHADHARI KIMBUNGA 'HIDAYA'

Na Asha Mwakyonde Dodoma 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama ameziagiza mamlaka za mikoa zitakazokumbwa na athari za kimbunga cha Hidaya kuendelea kuchukua tahadhari kuhusu kimbunga hicho.

Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), kutoa taarifa ya kimbunga hicho ambacho kinachokuja uelekeo wa Mashariki mwa Pwani ya Tanzania ambacho kimeendelea kuimarika na kusogea eneo la pwani mwa Tanzania.ambapo kikitarajiwa kuendelea hadi Mei 6, mwaka huu katika mikoa hiyo.

Akizungumzia leo Mei 3,2024 bungeni jijini Dodoma Waziri Mhagama ameitaka mikoa hiyo ni Dar es Salaam Mtwara, Morogoro Lindi, Pwani pamoja na Visiwa vya Mafia, Tanga na upande wa pili wa Muungano katika maeneo ya Unguja na Pemba.

Waziri huyo amesema kuwa wananchi wanaoishi katika maeneo yaliyotajwa na wanaojihusisha na shughuli mbambali baharini washauriwe kuchukua tahadhari ikiwa ni pamoja na kuendelea kufuatilia taarifa za utabiri zinazotolewa na TMA.

Waziri huyo amezitaka taasisi mbalimbali nchini pamoja na kamati za usimamizi wa maafa ngazi za mikoa, wilaya, kata, mitaa na vijiji kuendelea kuchukua tahadhari na kufuatilia taarifa za mamlaka hiyo.

"Kasi ya upepo ikiongezeka hadi kufikia kilometa 130 kwa saa na mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa baharini bado inaonyesha uwezekano mkubwa wa kimbuka kusalia katika hadhi ya kimbunga kamili hadi kufikia saa 12 zijazo ,"amesema Waziri huyo.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI