Na Asha Mwakyonde,Dodoma
MBUNGE Viti maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Rukwa Bupe Mwakang’ata amesema kuwa Mkoa huo una vijana na wanawake wengi wanaweza kulima vizuri changamoto hawana sehemu ya kulima.
Mwakang'ata ameomba programu ya Mradi wa Jenga Kesho iliyo Bora (BBT), uwafikie katika Mkoa wa Rukwa ili uwe ni miongoni mwa mikoa iliyopitiwa na mradi huo ambao unawanufaisha vijana na wanawake.
Hayo ameyasema leo Mei 3,2024 bungeni jijini hapa wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 amesema programu ya mradi huo umelenga mikoa ya Dodoma, Kigoma ,Mbeya, Singida, Pwani , Tanga, Njombe na Kagera huku akisema hajaona Mkoa wa Rukwa ambao ni miongonj mwa mikoa ambayo inalima na inaweza kulisha Tanzania nzima.
Pia mbunge huyo amempongeza Waziri huyo kwa kuwa na wazo la mradi huo ambapo vijana , wanawake na watanzania wanaenda kukumbolewa kiuchumi.
"Nichukue nafasi hii kumpongeza Rais wetu mama yetu Dk. Samia Suluhu Hassan kazi yake ni njema na ni nzuri hasa kwenye suala la kilimo amefanya mapinduzi makubwa tukiangalia asilimia 80 ya watanzania ni wakulima," ameeleza mbunge huyo.
Amesema Rais Dk.Samia amefikiria na kuweza kuweka ruzuku za pembejeo za kilimo huku akisema Rais huyo ameupiga mwingi hivyo apewe maua yake.
Mbunge huyo amempongeza Waziri wa kilimo Hussein Bashe pamoja na Naibu Waziri wake David Silinde kwa kazi nzuri ya ubunifu katika sekta ya kilimo huku akiwaombea wawepo kwenye nafasi hizo ili waendelee kuwatumikia watanzania.
Mbunge huyo pia amempongeza Katibu Mkuu wa wizara hiyo Gerald Mweli,Wakurugenzi na watendaji wa taasisi za KilimoKampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) ,Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA),Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania (CPB),Wakala wa Taifa wa Mbegu (ASA),Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB),Bodi ya Kotosho Tanzania (CBT).
Amesema taasisi nyingine ni Bodi ya Tumbaku Tanzania (TTB),Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) kwa pamoja wameweza kufanya kazi nzuri ndio sabubu ya wizara hiyo imekuwa kimbilio la wakulima.
"Awali wakulima wengi walikuwa masikini kwa sasa mkulima ni tajiri na tunakwenda kupata mabilionea wa sekta ya kilimo hii inatokana na uongozi mzuri kuanzia Rais, Waziri na watendaji wote katika sekta hii hongereni sana," amesema.
Akizungumzia suala la Pembejeo mbunge huyo amesema Mkoa wa Rukwa umepata pembejeo za kutosha na zenye ruzuku huku akisema wakulima wa Mkoa huo wanamshukuru Rais Dk. Samia pamoja na Waziri wa kilimo.
"Tumepata pembejeo za kutosha, mbolea za kutosha, tunaomba mwaka huu mbolea ziwahi kufika na ziwe za kiwango sawa tofauti na mwaka jana, pia nitakuwa mchoyo kama sijampongeza Mkurugenzi wa TFC kaka yangu Samwel Mshote na watendaji wote wamefanya kazi nzuri na wameweza kuleta pembejeo na mbolea nyingi," amesema.
Ameeleza kuwa Mkoa huo unaenda kuvuna mahindi kwa wingi Wizara imehamasisha kuhusu kulima na kwamba changamoto yao itakuwa ni soko huku akiiomba wizara kuzingatia masoko.
Mbunge huyo amesema Mkoa huo umepakana na nchi jirani ambazo tayari zina majang ya njaa serikali itakapo jiridhisha NFRA imenunua mahindi ya kutosha wapatiwe kibali ili waweze kuuza nchi jirani.
Amesema NFRA wamenunua mazo ya wakulima hao na kwamba changamoto ilikuwa kwenye mizani huku akiiomba mizani irekebishwe ili kutenda haki.
"Ndugu Mwenyekiti nizungumzie suala la mbegu , tunashuhudia mbegu zawenzetu kutoka nchini Zambia wakulima wengi wanazipenda zile mbegu sijajua za kwetu tatizo ni nini ," amehoji mbunge huyo.
Aidha ameiomba serikali kupitia wizara ya Kilimo kufanya utafiti ili mbegu zinazozalishwa nchini ziweze kuingia kwenye ushindani wa masoko.
Mbunge huyo pia ameomba mbolea zisiishie wilayani zifike hadi vijijini na kwamba ziweke kwenye viroba vya kuanzia kilogramu 5 hadi kilogramu 50 kwa kuwa Mkoa huo unawakulima wadogo, kati na wakubwa.
Katika hatua nyingine amesema kumekuwa na changamoto ya ushuru kwa wakulima anapoa mazao yake shambani tayari wataalam wanafika kutoza ushuru
0 Comments