EWURA YAWASHAURI WENYE MAGARI KUCHUKUA RISITI WANAPOJAZA MAFUTA


 Na Asha Mwakyonde,Dar es Salaam 

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imewashauri watu wenye magari wenye magari kuchukua risiti pindi wanapojaza mafuta lengo likiwa kurahisisha ulipaji fidia inapotokea magari yao yameharibika kutokana na mafuta waliyojaza yatakuwa na tatizo.

Akizungumza jijini hapa leo 11,2024 katika banda la mamlaka hiyo kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF),maarufu Saba Saba Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa EWURA, Titus Kaguo,amesema mteja akiwa na risiti hiyo ndani ya siku saba EWURA wanakwenda kupima mafuta hayo endapo yalisababisha gari kuharibika.

Kaguo amesema kuwa endapo EWURA itabaini tatizo la kuharibika kwa gari ya mteja linatokana na mafuta mwenye kituo atalipa gharama ya kukarabati gari hilo pamoja kuwapewa na adhabu.

“Watanzania wawe wanachukua stakabadhi, risiti kila wanapojaza mafuta ili iwe rahisi kupata fidia ya gharama ikitokea magari yao yameharibika kwa sababu ya mafuta yenye tatizo," ameeleza Kaguo.

Akizungumza gesi asilia ameeleza kuwa gesi hiyo imesaidia katika uzalishaji wa umeme nchini na kwamba inatumika kupikia katika baadhi ya taasisi, viwanda zaidi ya 50 Dar es Salaam na Pwani vinatumia.

Pia EWURA ina wanahamasisha watu wabadilishe mfumo na kuitumia gesi asilia iliyokandamizwa kwa kuwa inaokoa gharama ambazo zingetumika kwenye mafuta.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU