CBE YAJA NA KOZI YA 'MASTERS' MTANDAONI

Na Asha Mwakyonde,Dar es Salaam 

CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE),kimeanza kutoa masters kwa njia mtandao inakwenda kumrahisishia mtumishi kusoma bila kuathiri shughuli zake.

Haya yamesemwa jijini hapa katika banda la Chuo hicho kwenye maonesho ya 48 ya kimataifa ya Biashara dar es salaam ((DITF),

Mkuu wa Chuo cha CBE Profesa Tandi Luoga amesema mwanafunzi wa Masters anayesoma kwa njia ya mtandao , hahitaji kwenda mpaka CBE Mwanza,Dodoma Mbeya au Dar Es Salaam kusoma isipokuwa wakati wa mitihani ambapo mwanafunzi anaenda kwenye Tawi lolote la chuo hicho lililo karibu naye.

"Hatua hii imesaidia kusambaza elimu ya biashara ndani na nje ya Tanzania, lakini imepunguza gharama kusafiri na malazi kwa mwanafunzi husika." Amesisitiza

Pia amesema chuo hicho kina kozi nyingine nyingi kwa ngazi mbalimbali zikiwemo za mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi ambapo katika mafunzo ya muda mrefu wanaotoa elimu kuanzia ngazi ya cheti ,diploma,bachelor na Masters.

Aidha amesema mwanafunzi wa Masters anayesoma kwa njia ya mtandao , hahitaji kwenda mpaka CBE Mwanza,Dodoma Mbeya au Dar Es Salaam kusoma isipokuwa wakati wa mitihani ambapo mwanafunzi anaenda kwenye Tawi lolote la chuo hicho lililo karibu naye.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA