PURA YAJIPANGA KUONGEZA WAWEKEZAJI UTAFUTAJI GESI


Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam

MAMLAKA ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), imesema kuwa imejipanga kuhakikisha hatutakuwa na uhaba wa wa na kwamba wanatafuta wawekezaji wapya ili kuendelea kuwekeza katika eneo hilo.

Akizungumza jijini hapa leo Julai 11,2024 katika banda la PURA kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF), Mwenyekiti wa Bodi ya mamalaka hiyo Halfani Halfani

amesema wanajukumu la kutafuta wawekezaji hususan kwenye hl maeneo ambayo yako wazi lengo likiwa ni kutekeleza hilo.

Halfani ameeleza kuwa miradi ya serikali imekuwa ikizungumza kuwa inamuwekezaji ila mradi unaendelea vizuri kimazungumzo na kwamba endapo mazungumzo hayo yatafanikiwa wawekezaji wataweka mitambo pale Lindi, Likonko yakuchakata ges

Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa sheria ya mafuta inasema wawekezaji watafutwe kwa njia ya ushindani na sio kwa kuokotwa ili wapatikane kwa njia ya ushindani huku akisema kuna kitu kinafanyika ambacho kinaitwa Duru.

" Duru ni mkutano wa kutangaza maeneo husika ya miradi hivyo wanakuja pale kisha wanapewa utaratibu wa kuandika madokezo ya kuomba miradi," ameeleza.

Mwenyekiti huyo amebainisha kuwa Duru hiyo inaweza kufanyika labda robo ya mwaka ujao huku akisema Sheria ya mafuta ni kazi ya waziri kwa kuwa ndio mtaji wa leseni.

Akizungumzia majukumu mengine ya PURA ameeleza kuwa ina jukumu la kusimamia pale uuzaji wa gesi nje ya nchi utakapo anzishwa.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU