PURA YAWAHAKIKISHIA WANANCHI MATUMIZI YA NISHATI SAFI IFIKAPO 2034, ASILIMIA 80 KUTUMIA

Na Asha Mwakyonde Dar es Salaam 

MKURUGENZI Mkuu wa Mmamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA),Mhandisi Charles Sangweni, ameeleza kuwa watahakikisha ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya wananchi watakuwa wanatumia nishati safi yakupikia nchini.

Pia Mhandisi Sangweni amesema kwasasa wanatangaza maeneo mbalimbali ambayo kuvutia wawekezaji kwa ajili yakuja kushirikiana na taasisi pamoja na Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), kwenye kutafuta ambapo ikiwezekana kinachopatikana wakiwekee mkakati wa kukiendeleza.

Ameyasema hayo leo Julai 12,2024 katika banda la PURA, kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF), maarufu Saba Saba lengo kuweza kupunguza matumizi ya nishati na kutunza mazingira huku akisema serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ipo katika mkaka wa kuhamasisha wananchi kutumia nishati hiyo.

Mhandisi Sangweni ameongeza kuwa wanafanya tafiti mbalimbali za kuwezesha ili kuzalisha kiasi cha gesi ambacho kitaweza kuhudumia majumbani, katika magari na kwenye maeneo mengine.

Ameeleza kuwa hadi sasa kuna maeneo ambayo tayari yameshagunduliwa gesi ikiweno Mnazi Bay pamoja na Songosongo iliyopo Mtwara.

"Tutoke kwanye matumizi ya nishati ambayo inachafua hali ya hewa kama mikaa na kuni twende tukatumia nishati ambayo haina madhara kwa kiasi kikubwa," ameeleza . Mhandisi Sangweni.

"Shirika linaendelea na ugunduzi katika maeneo ambayo yana viashiria vya gesi ambapo imebainika ni asilimia 50 ya eneo la Tanzania na maeneo yenye viashiria ya mafuta SQM 5,034,000 karibu asilimia zaidi ya 50 za eneo la Tanzania," amesema.

Amefafanua kuwa wameshafanya tafiti SQKM 162 na kwamba eneo waliyofanyia utafiti mengi yapo Pwani kuanzia Kaskazini kwa maana ya Tanga, Kusini na Mtwara ambapo eneo hilo limeenda mbali kuingia baharini zaidi ya kilomita 400.

Mhandisi Sangweni amesema eneo hilo tayari wameshapata kibali Umoja wa Mataifa (UN),na kugawa katika vitalu, kwa kuanza ukanda huo wa Pwani watakuwa na vitalu ambavyo watavitangaza.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA