Na Asha Mwakyonde Dar es Salaam
MAMLAKA ya Serikali Mtandao (eGA), imezitaka Taasisi za Umma zihamasishe wadau wake ambao ni wananchi wanaowapa huduma watumie zaidi mfumo wa eMrejesho kuwasilisha maoni yao.
Pia mamalaka hiyo imejenga mfumo wa kubadilishana taarifa serikalini kwa maana ya mifumo kusoma kwa lengo la kurahisisha na kuboresha uwajibikaji seeikalini.
Akizungumza leo Julai 12, 2024 katika banda la eGA kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF), (Sabasaba), jijini Dar Dalaam Meneja Mawasiliano wa eGA Subira Kaswaga amesema Rais Dk.
Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza taasisi za umma kubadilishana taarifa kidigiti,hivyo wao kama mamlaka wametengeneza mfumo huo.
Amesema mfumo huo tayari wameshaunganisha mifumo mbalimbali na sasa ambapo wanachokifanya ni kuzihamasisha taasisi za umma ziweze kujiunga na mfumo huo ili ziweze kubadilishana taarifa.
Meneja huyo ameeleza kuwa suala la kujenga mifumo kwa ajili ya kurahisisha utendaji kazi katika utumishi wa umma ni jukumu la eGA huku akisema katika jukumu hilo imejengwa mfumo wa e mrejesho ambao ni daraja la.mawasiliano batons ya wananchi na Serikali.
Ameongeza kuwa hadi sasa taasisi ambazo zimeunganishwa na mfumo huu ni taasisi 141 na mifumo 148 imeshaunganishwa na katika hiyo mifumo 109 inasomana na kubadilishana taarifa.
Aidha amesema kuwa wananafanya jitihada mbalimbali ikiwa ni pamoja na ofisi za umma kuziunganisha kwenye mfumo huo na July 22-29 na kwamba waatarajia kuwa na kikao na taasisi za umma taktiban 70 kwa lengo la kuwapa elimu kuhusiana na mfumo huo lakini pia kuunganisha ili hizo taasisi zijiunge na mfumo huo wa kubadilishana taarifa.
0 Comments