TTCL YAPOKEA MAOMBI ZAIDI YA 200 WANAOTAKA HUDUMA YA FIBER

Na Asha Mwakyonde,Dar es Salaam 

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL), lililopo Viwanja vya Maonesho ya Mwalimu Nyerere maarufu kama Sabasaba kwa ajili yakuunganishwa na Fiber ya mtandao wa intaneti ambao ni nafuu zaidi.

Akizungumza katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni tanzu ya TTCL (T-PESA), Lulu Mkudde amesema katika maonesho hayo wanafanya shughuli mbalimbali ikiwemo kuandikisha watu ambao wanahitaji mtandao wa intaneti majumbani ama fiber.

“Tumepokea maombi mengi wateja wanahitaji huduma hii ambayo imeleta mapinduzi,yale malalamiko ya vifurushi vya intaneti kuisha haraka hapa hayapo,shirika limeleta huduma hii kumuwezesha mwananchi kutumia Internet bila kikomo,”amesema.

Amesema kupitia mitandao wamefungua milango ya kidigitali kwakuweka mazingira wezeshi kwa wananchi katika kutumia huduma za Interneti katika kutekeleza huduma mbalimbali kwa wananchi. shirika limefanya mambo mengi ikiwemo hiduma ya TTCL Pesa ambapo wamekuja na huduma ya akaunti portal ambayo inamwezesha mteja kufungua akaunti ya TTCL Pesa bila kuwa na hitaji la sim card.

Kwa hiyo anapodownload app ya T Pesa kupitia play store ana uwezo wa kufungua akaunti yake hata akiwa nyumbani na kufanya huduma zote za kifedha kwa njia ya kupitia app yake ya T pesa.

Akizungumzia kuhusu mkongo amesema mpaka sasa shirika linaendelea na mchakoto wa kufikisha huduma zake nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo ikiwa ni muendelezo wa kupeleka huduma hiyo kwa nchi za jirani. 

Amesema mpaka sasa huduma hiyo imefikishwa katika nchi nne ikiwemo Burundi,Rwanda,Zambia na Malawi.

Amesema kwa Tanzania ,Shirika limesambaza Mkongo wa Taifa katika mikoa yote nchini ambapo zaidi ya wilaya 98 zikiwa nazo zimefikishiwa Mkongo wa mawasiliano.

Mkudde amesema juhudi hizo zote zinalenga kuhakikisha juhudi za huduma za Elimu, Afya na Maendeleo ya kiuchumi ambayo yanatekelezeka kidigitali katika maeneo yote nchini.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA