Na Asha Mwakyonde,Dar es Salaam
CHUO Kikuu cha Dodoma (UDOM), kimepata tuzo ya mashindi wa kwanza kwa upande wa taasisi za elimu ya juu katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF),maarufu Saba Saba.
Pia Chuo hicho kipo katika mchakato wa kurusha Seteliti ambayo itasaidia kwenye mawasiliano.
Akizungumzia ushindi huo leo Julai13,2024 jijini Dar es Salaam katika maonesho hayo, Mkurugenzi wa Shahada za awali UDOM, Dk.Victor Marealle ambaye pia ni msimamizi wa maonesho kwenye banda la Chuo hicho amesema hiyo ni ishara ya kutambulika kwa kazi wanazozifanya kwa Chuo hicho.
Dk. Marealle ameeleza kuwa katika maonesho hayo wamekuja na bunifu mbalimbali za kitekinolojia ambazo zinafanywa na wanafunzi wao.
"Leo ni siku ya furaha sana Chuo kikuu cha Dodoma kwa kuibuka mahindi namba moja kwa upande wa Taasisi za elimu ya juu Tanzania," ameeleza Dk.Marealle.
Dk.Marealle ameongeza kuwa katika maonesho hayo wamekuja na baadhi ya bidhaa ambazo zimekuwa na maendeleo kutokana na kazi za wanafunzi hao huku akisema hiyo yote ni matunda yanayotokana na ufundishaji wao.
Amefafanua kuwa wanapowafundisha wanafunzi hao wahaishii kwenye nadharia bali wanaenda kufanya kwa vitendo ambavyo vinazalisha bidhaa hizo na kwamba hilo ni chimbuko la tafiti ambazo zinafanywa na wanafunzi hao kwa kushirikiana na wahadhiri wao.
0 Comments