PPRA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA SEKTA YA UTHBITI

Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam 

MAMLAKA A ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA),imeshinda tuzo ya mahindi wa kwanza katika kipengele cha mamalaka za uthibiti.

Pia Wadau,Taasisi za Umma na sekta binafisi wametakiwa kujiandaa kutumia Mfumo mpya wa Ununuzi wa Umma wa kielektroniki (NeST), kwa ajili ya michakato ya ununuzi wa Umma.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PPRA, Eliakim Maswi, Meneja Kanda ya Pwani wa mamalaka hiyo Vicky Mollel, leo Julai 13, 2024 katika banda Lao mara baada ya kupokea tuzo ya mahindi wa kwanza kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF), maarufu Saba Saba ameeleza kuwa wamepata mafanikio hayo kwa kuwa wameweza kuhudumia wateja zaidi ya 700 ambapo lengo lilikuwa ni kuhudumia wateja hao 500.

Meneja huyo ameongeza kuwa wameweza kutoa huduma kwa wateja mbalimbali zaidi ya 700.

"Tuna shukuru kwa mafanikio haya makubwa ambayo tuyapata katika maonesho haya kama PPRA tulijipanga kutoa elimu kwa ajili ya matumizi ya Mfumo wa NeST kutokana na Sheria mpya ya manunuzi ya Umma," amesema.

Meneja huyo amesema katika Sheria ya manunuzi ya Umma namba 10 ya mwaka 2023 kuna fursa nyingi kwa ajili ya Watanzania wajiandae kushiki fursa hizo ili kukuza uchumi wa Tanzania.

Amesema kuwa mamlaka hiyo ilitarajia ushindi kutokana na nguvu kubwa waliyoiweka katika kuhamasisha Umma na kwamba walihakikisha banda hilo linakuwa zuru la kuvutia wateja kupata huduma.

Mollel amefafanua kuwa siri ya mafanikio ya PPRA ni kufanya kazi kwa pamoja kama timu na kuweza kujituma.

Aidha amewataka wananchi wanaposikia maonesho wawe wanatembelea kwa kuwa kuna vitu vizuri yanayoandaliwa na PPRA kwa ajili ya wateja wao.

Meneja huyo ameeleza kuwa baada ya kupata tuzo hiyo watakuwa na msukumo makubwa wa kutoa huduma kwa wateja wao ikiwa ni pamoja na kujipanga kwa lengo la kuwafikia wateja zaidi hao.

Amesema wanatamani maonesho yajayo ya 49 waweze kuwahudumia wateja zaidi ya 2000.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI