PPRA: RAIS DK.SAMIA MGENI RASMI JUKWAA LA UNUNUZI WA UMMA AFRIKA MASHARIKI, WADAU WAKARIBISHWA


Na Asha Mwakyonde,DODOMA 

RAIS DK.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi Jukwaa la Ununuzi wa Umma la Afrika Mashariki ambapo limeratibiwa na serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA),

Tanzania fursa ya kwa mamalaka hiyo kuratibu Jukwaa hilo kwa mara ya nne ambalo linalotarajia kufanyika kuanzia Septemba 9 hadi 12 jijini Arusha mwaka huu na kutoa fursa kwa wadau mbalimbali wa ununuzi ndani na nje ya nchi pamoja na sekta za umma na binafsi.

Hayo yalisemwa leo Julai 18, 2024 jijini hapa na Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Eliakim Maswi wakati akizungumza na waandishi wa habari ameeleza kuwa mbali na ugunguzi huo Rais Dk.Samia atazindua mfumo Mfumo wa Ununuzi wa Umma wa Kielektroniki (NeST).

Amesema kuwa jukwaa hilo litawakutanisha wadau mbalimbali wa ununuzi wa umma na kutoa fursa ya kuwasilisha kero zao na kwamba juhudi zao katika kuboresha ni kujenga mazingira rafiki ya ununuzi wa umma katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Mkurugenzi huyo amesema watu1000 wanatarajiwa kuhudhuria jukwaa hilo na washiriki kutoka nchi za Tanzania,Kenya,Uganda, Burundi,Rwanda, Sudani Kusini, Somalia na Demokrasia ya watu wa Congo (DRC), kutoka sekta ya Umma,sekta binafsi ,Mashirika ya kitaaluma, Asasi za Kuraia na Taasisi za mafunzo.

"Jukwaa hili linaipa PPRA na wadau wengine fursa ya kuoata ujuzi na upashaji habari ambao ni muhimu kwa ajili ya kuendeleza uwazi, kujenga uelewa wa ununuzi kwa wadau,kuwapa maarifa na ujuzi," amesema Maswi.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo amesema faida za jukwaa hilo hapa nchini ni pamoja na kuimarisha ushirikiano, Uwazi uwajibikaji na ubadilishanaji wa uzoefu kati ya vyombo vya udhibiti wa ununuzi kutoka nchinwanachama wa Afrika katika utendaji kazi wa Serikali kwa kuboresha mifumo ya kitaasisi.

Mkurugenzi huyo amewaalika wadau mbalimbali kushirikia katika jukwaa hilo kwa ajili ya kupata uelewa na mambo mengi yanayohusu masuala ya ununuzi.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU