MWENYEKITI KARIAKOO AWATAKA WAFANYABIASHARA KUTEMBELEA BANDA LA TRA SABA SABA KUJIFUNZA

Na Asha Mwakyonde ,Dar es Salaam 

MWENYEKITI wa Jumuiya ya wafanyabiashara Kariakoo Martini Mbwana amewataka wafanyabiashara kutembelea banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),kujifunza na kujionea hali ya kibiashara.

Akizungumza leo Julai 5,2024 jijini Dar es Salaam alipotembelea banda la TRA katika maonesho ya 48 ya kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF), amesema kuwa kama mfanyabishara amezinguka katika banda la TRA ambapo amejionea vitengo tofauti tofauti ambavyo vinatoa huduma ikiwamo kuwapatia wananchi elimu juu ya masuala ya kodi.

"Nimekuja hapa kutembelea mabanda ya Saba Saba kujionea hali ya kibiashara Maonesho haya ni ya wafanyabiashara lakini pia na taasisi nyingine zipo," ameeleza Mbwana.

Aidha ameongeza kuwa amefurahishwa na mfumo ambao Rais Dk Samia Suluhu Hassan aliuahidi wa bandarini kwamba utaboreshwa na kupata maelezo ya kina huku akisema amejifunza vitu vingi.

Amewataka wafanyabiashara popote walipo nchi nzima hususan waliopo Mkoa wa Dar es Salaam wafike katika banda la TRA kujifunza ambapo kujifunza ni hatua kubwa ya kibiashara.

Mwenyekiti huyo amesema TRA wapo katika Idara zote wanatoa elimu na wanafundisha jamii na changamoto nyingine zinatatuliwa katika banda hilo.

Hata hivyo amewashauri wafanyabiashara kwenda kujifunza ambapo watagundua kuna tofauti kuwa kati ya kumfuata mtu ofisini kwake na kuja katika maonesho hayo.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI