WATAFITI UDSM WAOKOA MAZINGIRA, WATUMIA MAGANDA YA MATUNDA KUTENGEZEZA NISHATI MBADALA

Na Asha Mwakyonde Dar es Salaam 

WATAFITI kutoka Chuo Kikuu cha Dar esalaam(UDSM ),wamefanya utafiti wa maganda ya papai ,nanasi ,embe , tikiti maji na kupata bidhaa tofauti ambazo zinaweza kutumika kama mafuta ya taa,vitakasa mikono, nishati mbadala ya mafuta ya kwenye magari,spiriti na matumizi ya kwenye maabara.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF), Mtafiti kutoka chuo hicho Dk.Jovine Emmanuel ameeleza kuwa nchi inahamasisha matumizi ya gesi safi hivyo wao kama watafiti ni kuokuoa mazingira.

"Bidhaa hizi zinaenda sambamba na utunzaji wa mazingira kwani kinachotumika ni takataka ambazo huwa zinatupwa na muda mwingine zinachangia kuharibu mazingira.

Mtafiti huyo ameongeza kuwa bidhaa hiyo ipo tayari kwa matumizi kwa sababu imeshafanyiwa utafiti isipokuwa changamoto iliyopo ni mtaji wa kitengeneza bidhaa hiyo kwa wingi.

"Tunajua nchi io katika mkakati wa kutunza na kuokoa mazingira maganda ya matunda hayo huwa yanaoza na kusababisha uchafuzi wa mazingira lakini kupitia tafiti zetu tunayatumia hivyo tunatunza mazingira pia pamoja na kutengeneza bidhaa hizi," ameeleza Mtafiti huyo.

Ameeleza kuwa wanachukua takata za maganda ya matunda hayo na kutengeneza bidhaa ambazo ni muhimu kwa matumizi ya binadamu ambazo zinakuwa katika viwango tofauti.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI