NAIBU WAZIRI SAGINI ATEMBELEA BANDA LA BIMA LA CRDB, AIPONGEZA KUANZISHA BIMA YA KILIMO



Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam 

NAIBU Waziri wa Katiba na Sheria Jumanne Sagini ameishauri Kampuni ya bima ya Benki ya CRDB kutoa elimu ya bima ya kilimo (Agriculture insurance Company), kwa kuwa bima hiyo kwa kuwa ni kitu jipya kwa wakulima.

Haya ameyasema  Julai 5,2024 wakali alipowatembelea banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF), ameeleza kuwa benki hiyo imechelewa kujiunga na bima.

"CRDB mmechelewa kujiunga na bima lakini mnatupa faraja mlivyoamua kujiunga mnawagusa watanzania katika shughuli za kilimo na ufugaji.

Ameeleze kuwa anaamini benki ya CRDB kupitia bima hiyo itafanya vizuri endapo itakakazana watawapatia wananchi elimu ili wajue umuhimu wa kuchukua bima.

"Umezungumza Vizuri sana sana majanga yasiyo tarajiwa, mkulima anatoka analima anajua hali ya hewa inaruhusu baadae ukame unakuja mazao yanakauka yote, kama mafuriko yaliyokea Kilombero maeneo mengi ukipita kule utasema mpunga mwaka huu hawatapana lakini kama mmewawekea bima mkulima atavuna kwa kuwa bima hii inamjali,"amesema.

Awali Afisa Mauzo kutoka Kampuni ya bima ya Benki ya CRDB Angelina Kimweri ameeleza kuwa wanashughulika na bima zote za nyumba, gari, usafiri,Uhandisi pamoja na bima kubwa ya kilimo (Agriculture Insurance Company),kwa wakulima na wafugaji wote wanaopatikana nchini.

"Tunawakaribisha wananchi wenzetu waje kujiunga na bima hii kwa mahitaji ya bima yoyote ile kwa ajili ya kujikinga na majanga na maradhi yasiyo tarajiwa" amesema Afisa Mauzo huyo.

Aidha amewashauri wananchi kutembelea banda la CRDB ili kuweza kupata elimu na namna ya kujua bima hiyo inavyofanya kazi na kuweza kujikinga na majanga ambayo hayatarajiwi ikiwamo ukame mafuriko na magonjwa katika mifugo.

Kimweri ameeleza kuwa wananchi wameipokea bima ya kilimo na inaendelea kufanya vizuri huku akisema wao kama kampuni ya bima CRDB wanaendelea kutoa elimu kwa kuwa ni kitu jipya kwa upande wa wakulima ambapo wengi hawana uelewa wa bima hiyo.

" Tunafanya makadirio ya ulichokipanda katika shamba lako ili uweze kujikinga madhara yasiyo tarajiwa kama vile ukame, mafuriko hata ukipata hasara sisi kama bima tunaweza kukulipia" ameeleza Afisa masoko huyo.

Amefafanua kuwa wana bima kwa ajili ya mifugo ambapo wakati mwingine mifugo hiyo inapata magonjwa hivyo inapolipiwa bima inakingwa na maradhi yasiyo tarajiwa.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA