UDOM YAWAITA WAJASIRIMALI, WAFANYABIASHARA KUTENGENEZA TIBA LISHE


Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam 

CHUO Kikuu Cha Dodoma (UDOM),kimewata wajasiariamali na wafanyabiashara wa vyakula kufika katika Chuo hicho lengo likiwa ni kushirikiana kutengeneza tiba lishe na baadae kupata watu wa Tanzania wenye afya itakayowapeleka kwenye dira ya maendeleo ya mwaka 2050.

Akizungumza jijini hapa leo Julai 10,2024 katika banda la Chuo hicho kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF), maarufu Saba Saba Makamu Mkuu wa UDOM , Profesa Lughano Kusiluka, ameeleza kuwa chuo hicho kina utaratibu wa kutengeneza tiba lishe za kukabili magonjwa yasiyoambukiza.

Makamu Mkuu huyo amesema mpango wao kama Chuo ni kutafuta wadau na wabia waanze kutengeneza vyakula lishe ambayo ni tiba ili vipatikane kirahisi sokoni. 

" Chuo hiki kilikuwa cha kwanza kutoa shahada katika lishe tiba na chakula hivyo uzoefu huu umesaidia wataalam kutengeneza vyakula mbalimbali," amesema Prof. Kusiluka.

Prof.Kusiluka ameeleza kuwa mafunzo mengine yanayotolewa katika chuo hicho ni ya madaktari, wauguzi, wataalam wa lishe tiba, afya ya jamii.

Ameongeza kuwa Tanzania imejitangaza vizuri na ni nchi inayovutia kwa wawekezaji kutokana na juhudi zilizofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan na kwamba wanaunga mkono juhudi hizo za Serikali kwa kuandaa wataalam katika sekta mbalimbali.

Prof.Kusiluka, amesema Tanzania imejitangaza vizuri na ni nchi inayovutia kwa wawekezaji kutokana na juhudi zilizofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan na kwamba wanaunga mkono juhudi hizo za Serikali kwa kuandaa wataalam katika sekta mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU